March 5, 2020

JOTO limezidi kupanda kuelekea Machi 8 ambapo kutakuwa na mchezo kati ya Yanga na Simba uakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaja Martin Saanya mwenye ngome yake Morogoro ambaye ana beji ya FIFA atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo dhidi ya Yanga na Simba utakaopigwa majira ya saa 11:00 jioni.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, mwamuzi msaidizi namba 1 atakuwa ni Mohamed Mkono (Tanga), mwamuzi msaidizi namba 2 ni Frank Komba wa Dar es Salaam na mwamuzi wa akiba atakuwa ni Elly Sasii kutoka Dar es Salaam.

Katika mchezo huo pia kutakuwa na waamuzi wasaidizi wa ziada ambao ni Abdallah Mwinyimkuu kutoka Singida na Ramadhani Kayoko wa Dar es Salaam, wakati mtathmini wa waamuzi akiwa ni Sudi Abdi wa Arusha na kamishna wa mchezo atakuwa Mohamed Mkweche wa Dar es Salaam.


Kocha Luc Eymael amewahi kumlalamikia mwamuzi Martin Saanya kuwa aliinyima Yanga penalti katika mechi dhidi ya Mbeya City. Eymael raia wa Ubelgiji alimlalamikia Saanya kutotoa penalti baada ya Bernard Morrison kuchezewa rafu na mlinzi wa Mbeya City katika mechi ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1.

 Kwa Simba wakati Jonas Mkude akitolewa kwa kadi nyekundu msimu wa mwaka 2016 kwenye sare ya kufungana bao 1-1 alikuwa kati hivyo wote wana historia naye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic