March 1, 2020


SVEN Vandenbroeck,Kocha Mkuu wa Simba leo, Machi Mosi atakiongoza kikosi chake Uwanja wa Taifa dhidi ya KMC iliyo chini ya Harerimana Haruna.

KMC iliyopanda daraja msimu wa 2018/19 ina kibarua kigumu cha kutibua rekodi za Simba za kufuta uteja mbele ya Simba kutokana na kushindwa kushinda kwenye mechi tatu za Ligi Kuu Bara.

Simba na KMC, zimekutana mara tatu na mechi zote Simba ilikuwa ikishinda. Imefunga mabao sita huku KMC ikiwafunga Simba mabao mawili kwenye mechi zote.

Desemba 19,2018 Simba ilishinda mabao 2-1 mbele ya KMC Uwanja wa Taifa na Said Ndemla alifunga bao lake la kwanza ambalo analo mpaka sasa akiwa Simba na hajafunga lingine huo ulikuwa mchezo wa kwanza.

Aprili 25,2019 KMC ikikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Simba Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo wa Kwanza msimu huu uliochezwa Uwanja wa Uhuru Simba ilishinda mabao 2-0, leo kazi itakuwa nzito Uwanja wa Taifa kwa timu zote kusaka pointi tatu.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 62 na KMC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 21 zote zimecheza mechi 24

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic