March 1, 2020


DEAN Smith, Kocha Mkuu wa Aston Villa amesema kuwa ana imani na nyota wake mpya Mbwana Samatta atakuwa msaada kwenye kikosi hicho.

Leo Samatta ana kazi mbele ya Manchester City kwenye mchezo wa Kombe la Carabao utakaopigwa majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Wembeley.

Smith amesema:"Samatta ana vitu vingi alivyonavyo licha ya kuwa ni mpya na anaona namna ligi ya huku ilivyo, namtambua ana juhudi ila nimemwambia aongeze juhudi zaidi ya hapo," .

Villa imetinga hatua ya fainali baada ya kuinyoosha kwa mabao 2-1 Leicester City na kupenya kwa ushindi wa mabao 3-2 kwani mchezo wa kwanza zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic