MABINGWA watetezi wa Kombe La Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool Jana wamevuliwa ubingwa kwa kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Atletico Madrid.
Kichapo hicho wamekipokea kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Anfield na kufanya wasiamini walichokiona kutokana na kuamini kwamba walikuwa na nafasi ya kupindua meza kibabe baada ya mchezo wa Kwanza kuchapwa bao 1-0 ugenini.
Jumla wanatolewa Kwa kuchapwa mabao 4-2 na wapinzani wao hao Atletico ambao wanasonga hatua inayofuata ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Walianza kupata matumaini walipofunga bao la kwanza dk ya 43 kupitia kwa Georginio Wijnaldum mambo yakawa magumu zilipoongweza dk 30 ambapo bao lao walilofunga dk ya 94 lilijibiwa na Atletico Madrid kupitia kwa Marcos Liorente dk 97 alikomelea msumari wa mwisho dk ya 105+1.
Lile la pili Kwa Atletico Madrid lilifungwa na Alvaro Morata na kuipoteza mazima Liverpool kwenye reli iliyo chini ya safu ya ulinzi inayoongozwa na Van Dijk
0 COMMENTS:
Post a Comment