March 12, 2020

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa sababu kubwa ya kumpa kandarasi nyota wake Mudhathiri Yahya ni pendekezo la Kocha Mkuu Arstica Cioaba ambaye ni mkuu kwenye benchi la ufundi.

Nyota huyo ameongeza kandarasi ya miaka miwili hivyo atabaki ndani ya Azam FC mpaka 2022.

Msimu huu wa 2019/20 Mudathir ametupia bao moja ndani ya kikosi cha Azam FC wakati wakisepa na pointi tatu jumla mbele ya Polisi Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru kwa shuti la nje 18 akimalizia pasi ya Nicolas Wadada.

 Abdulkarim Amin CEO wa Azam FC amesema kuwa mpango mkubwa ni kuwapa nafasi wazawa ndani ya kikosi hicho jambo litakaloleta ushindani mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic