March 12, 2020


MARCEL Kaheza, mshambuliajai wa Polisi Tanzania amesema kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu unawafanya wakomae kusaka matokeo kwenye mechi zao zote ili kujiweka kwnenye nafasi nzuri.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa wamekuwa wakikutana na timu ngumu ambazo zina uzoefu mkubwa ndani ya ligi ila kutokana na maelekezo wanayopata yanawafanya wajiamini wakiwa ndani ya uwanja.

"Kiukweli kwa sasa ligi sio nyepesi ukizingatia kwamba timu nyingi zinashuka daraja, kila mechi kwetu ni fainali tumekubaliana kufanya kazi kwa juhudi na hicho ndicho tunachokifanya tukiwa uwanjani," amesema.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 42 imecheza mechi 28, mchezo wake uliopita ililazimisha suluhu mbele ya Mtibwa Sugar ikiwa uwanja wake wa nyumbani Ushirika,Moshi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic