March 5, 2020

ZIMEBAKI siku tatu kuwakutanisha  Yanga na Simba Uwanja wa Taifa kwenye mechi nne za hivi karibuni ambazo ni dakika 360 Yanga imeipoteza Simba kwa kucheza mechi hizo bila kuruhusu bao.
Safu ya Yanga ya ulinzi inayoongozwa na Lamine Moro pamoja na Juma Abdul imeonyesha ukomavu kwa kuipoteza ile ya Simba inayoongozwa na Pascal Wawa sambamba na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Yanga imecheza mfululizo bila kuruhusu bao ilikuwa ni Februari 23 mbele ya Coastal Union 0-0, Februari 26,Gwambina FC 0-1 huu ulikuwa ni wa FA, Februari 29 Alliance 0-2 na Machi 3, Yanga 2-0 Mbao FC. Simba ndani mechi zao nne ambazo wamecheza mfululizo kabla ya mechi ya jana dhidi ya Azam FC walifungwa mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 3-1, Februari 22, dhidi ya Biashara United, Februari 25 waliruhusu bao kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Stand United kwenye sare ya kufungana bao 1-1, ila walishinda kwa penalti 3-2 na kutinga hatua ya robo fainali.
Februari 18 haikufungwa mbele ya Kagera Sugar ikishinda bao 1-0 na Machi Mosi haikufungwa na KMC wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kwenye mechi hizo nne mfululizo Yanga imefunga mabao matano bila kuruhusu bao na Simba imefungwa mabao mawili na kufunga mabao sita.

4 COMMENTS:

  1. Vipi imeipoteza Simba, imefanya hesabu vizuri? Ni hivi Yanga iliishinda timu dhaifu inayoshuka daraja mbili kwa Bila na Mnyama aliishinda timu kali iliyokamilika kila idara taratibu ya pili baada ya Mnyama inayogombea ubingwa tatu kwa mbili. Pima hayo

    ReplyDelete
  2. Mwandishi mbona unajichanganya tu, hueleweki. Simba kapotezwa kivipi? Toa takwimu Vizuri

    ReplyDelete
  3. Uchambuzi mbovu na mchambuz mbovu

    ReplyDelete
  4. HIVI HUYU JEMBE ANATUFANYA SISI MAFALA. KASOMA UANDISHI WAPI?UTUMBO TUU DUUU TUMECHOKA. ILE JANJA JANA YA VICHWA VYA HAVARI BASIKUMDANGANYA MSOMAJI IMEPITWA NA WAKATI,KAWADANGANYE VYURA HUKOOOO MATOPENI.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic