KESHO Yanga itakuwa na kazi ya kusaka ponti tatu mbele ya Mbao FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa1:00 usiku.
Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wanachohitaji ni mwendelezo wa ushindi kwenye ligi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa amekuwa akikitazama kikosi chake kwa muda mrefu na kukifanyia marekebisho pale kinapokwama ili kuwa bora.
"Nimekuwa nikifanya kazi kwa ukaribu na wachezaji wangu na kuona namna gani tunakuwa bora, tuna mechi nyingi ambazo zinatukabili na zote ngumu tunachokifanya ni kuona namna gani tutapata matokeo.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwani uwezekano wa kupata matokeo upo na uwezo upo mikononi mwa wachezaji," amesema.
Yanga ipo nafasi ya nne ikiwa imecheza mechi 23 ina pointi 44 kibindoni.
Anamweli chura ni chura tu
ReplyDeleteBado anawaza ubingwa duuu.Ama kweli ile methalali mwenye macho aambiwi tazama kwa vyura mmmm
Kenge hajui kaumia mpaka aone damu!!!
ReplyDeleteHata chura anapenda sana kwenye maji lakini sio ya moto wala ya baridi sana,cha ajabu kwa chura ukimtumbukiza kwenye maji ya baridi kisha ukayabandika jikoni kaa ukijua chura hatoki mpaka ataiva maana ufahamu wake ni mdogo,hao ndio chura tena wapo wa aina nyingi sana makundi kwa makundi hata ughaibuni wapo chura kama hawa hapa kwetu,asante mungu kwa ufahamu ulionijalia,maana ingewezekana kuumbwa chura basi leo nami ningekua miongoni mwa chura wanaochemshwa bila wao wenyewe kujua,chura unakwama wapi??pole sana.
ReplyDeleteILI CHURA UCHUKUE USHINDI LAZIMA USHINDE MWECHI ZAKO KARIBIA ZOTE ULIZOBAKIZA,NA WAKATI HUO UNATAKIWA UMUOMBEE SIMBA APIGWE MECHI TANO AU SITA,MAANA AMEBAKI NA MECHI 13 AKISHINDA 8 UMESHAUKOSA UBINGWA HATA USHINDE MECHI ZOTE HUTAWEZA KUMFIKIA.USHAURI WA BURE PAMBANA NA ASFC LABDA UNAWEZA UKAAMBULIA CHOCHOTE KITU ILA KWA LIGI KUU NAKUSHAURI JIPANGE MSIMU UJAO MTANI,KWASABAU NI NGUMU KWA SIMBA KUPOTEZA MECHI SITA YANI ALAMA 18 ILI AUKOSE UBINGWA HAPO HAPO NI RAHIS SANA KWA YANGA KUENDELEA KUPIGWA NAKUPOTEZA MECHI,KIBARUA CHA NAMUNGO,KMC,AZAM,SIMBA SIO CHA MCHEZO.
ReplyDeleteNa hata tarehe 8 keshokutwa tusipojipanga simba atatufunga magoli mengi sana,tunaomba kazi ifanyike kama ilivyofanyika round ya kwanza tuwamalize mapema sana kwakutumia mbinu za nje ya uwanja vitambaa vyekundu,mayai,na vyungu vipya ili kazi iende sawa mapema kinyume na hapo tutakimbia lazima watatupiga hawa jamaa kwa mpira qanaocheza sasaivi huyu konde boy na yule kanda wangepigwa mashine kama kagere maana hao ndio watasumbua sana mzamiru kwisha habari yake,miraji athumani ndio kabisa,kamat ya roho mbaya fanyeni kazi yenu huyu konde boy atatuhanisi huyu kwann asipigwe mashine mapema tu,tunaomba majibu plz tunaumia sisi mashabiki tani tunaumia sana jamani tusaidieni kwa hilo.
ReplyDeleteMimi nawaomba vyura msibabaike wala kuvunjika moyo, tieni Pamba mashikioni msisikie la yoyote muendelee na kampeni zenu mujuwe kuwa Ubingwa ni wenu tu madhali munautaka cha muhimu pia mumsikilize mganga kwa kila akitakacho na matunda mtavuna na kuinyamazisha mikia.
ReplyDelete