March 12, 2020


JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa anaamini katika uwezo wa nyota wa Simba, Said Ndemla licha ya kwamba hajamuona kwa muda mrefu.

Abdul amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao amekuwa akiwafurahia wawapo ndani ya uwanja ni pamoja na Ndemla.

"Ni mchezaji mzuri akiwa ndani ya uwanja anajituma na uwezo wake ni mzuri, kwa sasa sijamuona akiwa ndani ya uwanja kwa muda mrefu ila nina amini akipata nafasi atafanya vizuri," amesema.

Ndemla amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Simba kwenye mzunguko wa pili Simba ikiwa imecheza mechi tisa hajacheza mchezo wowote.

5 COMMENTS:

  1. Na hata pindi mkimpata mjuwe Roho yake yote itakuwa kwa kule alipolelewa na kukulia, ni kama vile kumuowa mwanamke aliyeachwa na roho yake yote ipo kwa mume wa Kwanza

    ReplyDelete
  2. Mmrzidi kuzungumzia wachezaji wa simba

    ReplyDelete
  3. Mbona Ajibu amekulia simba lakini yanga aliupiga mwingi kuliko kwa mkia tulia mkia.

    ReplyDelete
  4. Mbona Ajibu amekulia simba lakini yanga aliupiga mwingi kuliko kwa mkia tulia mkia.

    ReplyDelete
  5. eti kumzungumzia sasna mchezaji wa simba. acheni roho mbaya sasa kama mchezaji wa simba akifanya vizuri asipewe sifa? roho za kishetani na wivu zinaturudisha nyuma sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic