April 11, 2020

UONGOZI wa Yanga
umesema kuwa hauwezi kushindwa kuinasa saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama iwapo watahitaji kumpata.

Kumekuwa na tetesi za Yanga kuiwinda saini ya Chama raia wa Zambia ambaye ana uwezo wa kubadili matokeo namna anavyotaka ambapo aliweza kufanya hivyo kwenye mechi mbili za kimataifa msimu wa 2018/19 mbele ya Nkana FC na AS Vita kwa kufunga mabao ya usiku.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mpango mkubwa wa kuboresha kikosi chao upo na kutokana na uwepo wa kampuni ya GSM  hawashindwi kumpata mchezaji yoyote.

"Tunajua kwamba mashabiki wana shauku ya kuona kikosi bora na makini lengo letu ni kuwa na kikosi ambacho kitaleta ushindani hivyo ikiwa tutamhtaji huyo Chama haitakuwa kazi kumpata kwani kila kitu kinawezekana.

"Hatuna mpango wa kumfuata Zambia kwa sasa kwani mambo yamebadilika na mawasiliano yapo hivyo ni suala la kumalizana moja kwa moja ni suala la kusubiri," amesema.

Chama kwa sasa yupo Zambia ikiwa ni kwa ajili ya mapumziko ya kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

6 COMMENTS:

  1. Kila la kheri. Ila mtu unawezaje kujipa moyo kuwa kila kitu unaweza ili hali unategemea hela ya mtu mwingine? Akibadili mawazo jee?

    ReplyDelete
  2. Tena mtu mwenyewe kawekwa na viongozi ndiyo sababu uongozi unathubutu kufukuzana kukidhi matakwa ya "big boss"

    ReplyDelete
  3. Chama akitoka timu kubwa hawezi kwenda timu ndogo ambayo kushiriki mashindano ya afrika mpaka mbeleko

    ReplyDelete
  4. Sawa wazee jipeni moyo sio vibaya,hela hazina mwenyewe hilo si mnajua.

    ReplyDelete
  5. Daima mbele nyuma mwiko. Pongez kwa uongoz uliopo madalakan

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic