KAMA lengo
ni kushinda mataji na kupata mshahara kwa wakati, Simba ni sehemu sahihi sana
kwa Papy Tshishimbi. Tangu tajiri, Mohammed Dewji aliporejea ndani ya timu hiyo,
suala la madai ya wachezaji halipo tena ndani ya Msimbazi.
Hakuna
mchezaji anayedai posho wala mshahara wake, wote wanalipwa kwa wakati. Hakuna
kiongozi yeyote anayedai, wote wanalipwa chao mapema tu.
Tangu Mohammed
Dewji amerejea Simba, timu yenye ushindani imetengenezwa na mataji sasa imekuwa
ndiyo utamaduni wa mnyama kwa misimu miwili mfululizo.
Kama Papy
Tshishimbi anataka pesa kwa wakati na kuwa sehemu ya timu iliyoshinda mataji
hata kama ukiwa benchi, Simba ni chaguo sahihi.
Kwa sasa ni
rahisi kushinda mataji hata kama ukiwa benchi kuliko kuwa sehemu ya kikosi cha
kwanza cha Yanga. Moja kati ya kazi ngumu ambazo anaweza kukutana nazo
Tshishimbi ni kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.
Hili suala
gumu mno. Papy ni moja ya viungo wazuri sana lakini Simba ina wachezaji wa
nafasi yake wengi na wazuri zaidi yake. Ndiyo, wako wengi na wazuri zaidi yake.
Anaweza kucheza lakini atatakiwa kupambana sana.
Misimu
miwili iliyopita Simba wametengeneza kikosi cha ushindani hasa. Karibu kwenye
kila nafasi kuna wachezaji wawili wanaokabiliana kwa ubora.
Idara ya
kiungo anakocheza Papy ndiyo hakufai. Kila mtu fundi. Ndiyo, anaweza akacheza
lakini itamuhitaji ajitoe sana na bahati mbaya pia umri wake unakwenda. Yuko juu
ya miaka 30, bidii sana inahitajika.
Unapoona
watu wenye kiwango kama Sharaf Shiboub anakalia mkeka, fundi kama Hassan
Dilunga anasugua Mbao haiwezekani Tshishimbi akapata urahisi wa kuingia moja
kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.
Simba kwa
sasa inahitaji mchezaji mwenye kitu cha zaidi ya Clatous Chama na Jonas Mkude
ambacho sikioni kwa Papy. Sidhani Kama zinaweza kuwa mbinu nzuri za kuimarisha
timu kwa kumleta Tshishimbi labda kama inatumika kuwakomoa Yanga.
Sina tatizo
na ubora wa Tshishimbi, ni mchezaji mzuri na ana msaada mkubwa pale Yanga
lakini sidhani kama atatoboa kwenye kikosi cha kwanza. Kwa aina ya wachezaji
waliopo pale Simba wa idara ya kiungo, sidhani kama atawaletea kitu cha
tofauti.
Kama malengo
ya Tshishimbi ni kupata pesa na kulipwa mshahara wake kwa wakati, Simba ni
sehemu sahihi sana kwake na hasa kwa kipindi hiki, lakini kama lengo ni kuwa
sehemu ya kikosi cha kwanza, basi pale sio.
Simba ina watu
wengi na bora kwenye eneo hilo. Kama kupata muda kidogo wa kucheza sio tabu
kwake, Msimbazi itamfaa sana.
Haruna
Niyonzima alikuwa mchezaji hodari na tegemeo sana ndani ya Yanga, lakini
alipokwenda Simba kwenye zama hizi alishindwa kupata nafasi. Baada ya kurudi
Yanga, amekuwa tegemeo tena. Yanga bado ushindani ni mdogo sana.
Sio kwamba
Haruna hakuwa bora ndani ya Simba, hapana lakini haikuwa rahisi kwake kuwa
sehemu ya kikosi cha kwanza. Ibrahim Ajibu alikuwa mchezaji bora na tegemeo kwa
Yanga kwa misimu yote miwili akiwa huko, lakini aliporejea Simba, amekuwa mtu
kula mkeka tu.
Pia sio kwamba
Ajibu ni mchezaji mbaya au ameshuka kiwango, hapana. Ajibu bado ni yule yule
isipokuwa kwa sasa kuna kina Ajibu wengi sana pale Msimbazi.
Sina tatizo
kabisa na uwezo wa Tshishimbi, ni mchezaji mzuri lakini nadhani Simba kuna
wachezaji wengi sana wa ubora wake na zaidi. Kama Tshishimbi anatafuta pesa ya
uhakika, pale Simba ipo. Sina wasiwasi na uwezo wake, nina wasiwasi na yeye
kupata nafasi ya kwanza kwenye kikosi.
Kupanga ni
kuchagua, kuna muda mchezaji wa soka anahitaji pesa na kuna muda anahitaji
kucheza. Kuna muda mchezaji anahitaji kushinda mataji, kazi kwa Tshishimbi tu.
Pale kumekuwa na changamoto nyingi sana nje na ndani ya uwanja.
Sio rahisi
kupata pesa na mataji kwa msimu huu lakini unaweza kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.
Yanga bado inapambana kuimarisha kikosi chake. Kama watajipanga vizuri kiuchumi
na kiufundi wanaweza kushindana haswa kuanzia msimu ujao.
Misimu
mitatu mfululizo, unaonekana imekuwa na ufalme wa Simba. Simba wana timu bora,
hawana tatizo la kuhudumia timu. Tshishimbi anapaswa kuchanga vema karata yake.
Ni muda wa
kujipanga haswa. Bado anaweza kucheza Yanga kwa misimu mingine hata mitatu,
lakini akienda Simba na kuchemsha haiwezi kuwa rahisi kwake kurudi Yanga kama
ilivyokuwa kwa Niyonzima.
Kuna tofauti
kati ya ufalme wa Niyonimza na ufalme wa Tshishimbi pale Jangwani. Bado Tshishimbi
hajazikonga hasa nyoyo za wapenzi wa Yanga.
Amekuwa na
timu kwa misimu miwili na nusu sasa na hajashinda ubingwa wowote. Bado hajaacha
alama pale Jangwani. Jina lake ni rahisi sana kufutika kuliko la Niyonzima.
Huu ndiyo
wakati wake wa kuamua. Huu ndiyo muda wake wa kuchanga karata zake vema.







this post has too many repeatative words....be professional mzee
ReplyDeleteword
DeleteHaahaaa He is trying inderectly to beg Tshishimbi not to leave Yanga...too much ngonjera.Is Tshishimbi decision and not us.
DeleteAende simba akajaribu bahati yake mpira pesa
ReplyDeleteSimba hamna mpira pale. Kama uongo wacheze Iyo klabu bimgwa wanatoka asubui tu.Ila Tff na marefa wanaibeba kwenye ligi
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
DeleteKweli hapana mpira na ndio mana wakafika robo fainali ya ubingwa wa Africa na kwani ni nani aliecharazwa tatu Bila na Kagera Sugar na aliekimbiwa kwa kushindwa kulipa mishahara isipokuwa gongowazi. Anakitaka mchezaji mwenye akili timamu ni kupata chake kwa hakika na wala sio kupata nafasi ya kucheza I kwasababu lengo la kila mchezaji ni kupata kipato cha hakika kuendeshea maisha yake na mchezaji mwenye kiwango lakini kazidiwe na wengine hasugui mbao maisha kama tulivo on a kwa Manulna alipoumia Kakolanya aka chukuwa pahala pake na Gerdial Michel alipoumia MO na pia Dilunga na Shibob na pia alipoumia Kapombe na wengi wengineo
ReplyDeleteUmeshindwa kuelewa kuwa kuwa Niyo kilichomsimbua ni majeruhi na aliporudi kwa mechi alizocheza Nazi ilionekana. Ajibu hata angekuwa Yanga leo asingekuwa mfalme, ana ball control na pasi zenye macho Ila yuko slaw sana anauwa motion ya team. Kwa BM33 asingefua dafu. Gadiel na Shabalala hawana tofauti ila Shabalala ni mtoto wa nyumbani. Tshishimbi yuko sawa ila kwenda Simba itakauwa kosa kwake na kwa simba, kwanza atawapunguzia nafasi za wachezaji was kigeni wakati hana kipya anachoweza kuongeza. Lakini pili hawezi kufanya yale anayofanya akiwa Yanga kwakuwa ile heshima ya free role na command aliyonayo Yanga hawexi kuipata akiwa Simba kutokana na ugeni kwenye kikosi. Kwa shishimbi mwenyewe thamani yake itashuka kutokana na kutocheza kwa kiwango mile na hivyo atalazimika kwenda kwa akina ndanda kupandisha kiwango. Issue ya maslahi sioni kama ni kigexo kwakuwa pia Yanga kwa sasa wana GSM ambaye amesolve issue ya ukata. Labda kwa ubingwa was mwaka huu, yes lakini pia yeye hawezi kuwa sehemu ya ubingwa huo. Kwa mwakani I doubt, maana kilichombeba Simba mwaka huu ni mapungufu ya Yanga ambayo bado siyaoni kwa mwakani unless kutokee changes zinaxoweza kutokea popote.
ReplyDeleteNimependa uchambuzi. Uko vizuri. Washauri na wengine wenye nia hiyo.
ReplyDeleteMapungufu ya yanga ndiyo yaliyombeba simba??hivi uko sawa kweli??kwahyo sasaivi yanga haina mapungufu??mbona imefungwa na kmc baada na bado ikasuluhu na namungo nipe sababu brother??unajua usiandike kishabiki maana utaumbuka muda utakapofika,kumbuka mpira ni mchezo wa makosa,mistake ndogo sana in english we call it an eror(small deviation from true value)unaweza ukafanikiwa kulifanya jambo lakini sio kwa ufanisi unaotakiwa na hatimae linakuja kukuletea matokeo hasi katika mazingira,hapa tusiangalie simba wala yanga kwasababu yeyote anaweza akaangukia hapo,isipokua penye ukweli lazima tuongee kama unaamin kwamba kuna miujiza basi qmin kwamba hata uchawi upo,na mpira wa bongo kamwe hauwezi kusogea kwa staili tunazofanya sisi,kama yanga wangekua wanajielewa basi wasingefanya ujinga wa aina hii wakukamia mechi ya simba alafu angalia kilichomkuta baada ya mechi haina haja yakusimulia maana kila mtu anajua,sasa unapokuja na hoja kwamba simba walibahatisha kwasababu yanga walikua na mapungufu ambayo tayari yameshafanyiwa kazi kwanini walifungwa nakusuluhu baada ya dabi??bado nafasi ya simba ni kubwa sana kwenye klabu bingwa Afrika hata ukatae ila ukweli ndio huo,yanga bado sana jaribu kuichunguza yanga utagundua tatizo liko wapi,najua utajitoa ufahamu ila kilichoibeba yanga mbele ya simba ni uchawi na kukamia mechi hakuna lolote la ziada,povu ruksaaaa.
ReplyDeleteSidhani kama viongozi wa Simba wana nia kweli ya kumsajili. Ninachokiona kwa sasa kila mchezaji wa Yanga ambaye hajasajiliwa na GSM na analipwa mshahara na uongozi anaitaja sana Simba ili GSM waingilie kati wampe mkataba mnono. Kwa hili Tshishimbi kashafanikiwa kwani GSM wameshamwita mezani. Alianza huyu Tshishimbi na juzi kati nimemsikia tena Makapu. Naamini na wachezaji wengine wa Yanga watatumia gia hiyo hiyo.
ReplyDeleteOnyo tunaomba radhi kwa wale wanaotamani kutukana hatutapokea matusi ila povuu ruksaaaaaa.karibuni sana.
ReplyDeletemtoa hoja ameonyesha mapenzi yake kwa Simba badala ya kutueleza sababu za kwanini Tshishimbi asibaki Yanga....tatizo hili wahariri wetu kuwa na mahaba na timu fulani linaleta shida pale wanapotakiwa kutoa habari wao wanaonyesha mahaba kwa timu
ReplyDeleteMtoa hoja kaeleza vizuri sana, pengine kumuelewa ni kazi maana utakuwa umepambwa na mahaba ya timu fulani lakini ukisoma kwa undani utamuelewa, na ndo maana Yanga wanamtaka Demla lakini kiukweli Yanga ikikamilika ikasajili bila magumashi sioni nafasi ya Demla wa Fei toto ila kwa kuwa kikosi bado wanajaribu kukisuka ndo maana hawa wanaonekana bora sana, lakini kiukweli Yanga inahitaji maboresho mengi sana lakini simba wanahitaji replacement chache sana kwa ajili ya kuziba nafas za wachezaji tena umri
ReplyDelete