MAPAMBANO lazima yaendelee kwa sasa licha ya kwamba kuna Virusi
vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.
Virusi hivi ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19 inabidi
tukubali kwanza kwamba vimeleta mtikisiko kwenye ulimwengu wa michezo pamoja na
sekta nyingine ambazo zimekuwa zikiathirika pia.
Tunaona kwamba ile burudani ya Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda
na pia hata kule kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza kila kitu kimesimama
kwenye familia ya michezo vingi tunakosa.
Nguve kazi inapungua kutokana na vifo ambavyo vintokea ila haina
maana kwamba nasi lazima tuwe na hofu kubwa hapana tuamini kwamba kila kitu
kitakuwa sawa hapo baadaye ila tusiwe na
hofu ya kupitiliza.
Agizo la Serikali lisipuuziwe kwa kuwa hakuna kiongozi
anayependa kuona watu anaowaongoza wanapita kwenyye matatizo ni lazima achukue
hatua ili kuwaweka salama watu wake.
Ikumbukwe kuwa Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, Machi 17 alizuia
masuala yote ya mikusanyiko isiyo ya lazima na kusimamisha shughuli zote za
michezo kuanzia Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Wanawake.
Bado hatujatoka huko kwa sasa tunapaswa kuendelea kupambana kwa
pamoja kila mmoja kwa wakati wake na hapo ndipo tutaweza kuuthibitisha ule
usemi wa kwamba umoja ni nguvu.
Afya ni kitu cha msingi kwa wana familia ya michezo pia kumlinda
mwanamichezo mwenzako pia ni muhimu tusichukulie utani kwa sasa.
Tukiachana na masuala ya Corona ambayo nimuhimu kukumbushana
hasa kwa nyakati hizi leo ningependa nizungumzie kuhusu mipango ya wachezaji na
timu kiujumla.
Tunaona ligi zote zimesimama kwa wakati huu ni muhimu kuchukua
tathimini ya wapi ambapo timu ilikuwa ikishindwa kufanya vizuri kisha dawa
ianze kutafutwa kwa wakati huu.
Kinachotakiwa kufanya kwa sasa ni kutumia mapumziko haya ya
lazima kwa ajili ya kutafuta nguvu mpya ya kumaliza ligi iwapo hali itatengamaa
kwani hakuna ambaye anajua kwamba lini ligi itarejea.
Kuna timu ambazo mpaka sasa hazijawa na dira nzuri kutokana na
kuwa na matokeo mabovu hivyo muda wao wa kutafuta pale ambapo walikwama mwanzo
wa msimu kutafuta majibu ya makosa yao.
Ni ngumu kufanikiwa kwa asilimia kubwa kwa kuwa timu nyingi
zimevunja kambi lakini kuna namna itakayowafanya mtambue kwamba kuna sehemu
ambayo mlikuwa mnakosea lazima muifanyie kazi.
Kuna makocha ambao walikuwa wanaeleza kuwa wanshindwa kupata
matokeo kutokana na wachezaji wao kuchoka hasa kwa kusafiri muda mrefu basi ni
muda wa kuwapa wachezaji mapumziko.
Pale ambapo watakuwa na muda mwingi wa kupumzika iawafanya
watatue lile tatizo la uchovu na watarudi wakiwa kwenye nguvu mpya na mtazamo
mwingine.
Zipo timu nyingine ambazo ushindi wao ulikuwa unategemea baadhi
ya wachezaji lakini wameshindwa kufikia malengo kutokana na aina ya mfumo wa
kocha, katika hili pia ni lazima kutafuta suluhisho.
Kocha lazima atazame upya aina ya wachezaji alionao ili
kuwajenga upya na kuwatengeneza muunganiko mzuri ambao utampa nafasi ya kupata
matokeo anayohohitaji.
Muda huu pia ni wakati wa kuwakumbusha wachezaji kwamba muda wa
kubaki ndani ya ligi unakaribia kumeguka hivyo lazima wapambane ili kulinda
nafasi zao ambazo wapo.
Wasisahau kwamba kuna timu nne ambazozinashuka daraja msimu huu
hivyo kushindwa kuchukua tahadhari mapema itakuwa ni hasara kwa timu iwapo
itaweza kushuka daraja.
Matokeo mazuri hayaji kimiujiza ama kwa kuongea tambo nyingi
kabla ya mechi hakuna kitu kama hicho ni lazima kuwe na mipango na mbinu
makini.
Timu ambayo itashindwa kufanya mipango vizuri itarejea na
kuonyesha kile kilichokuwa kinafichwa hadharani ambapo kila mmoja atajua
kupitia matokeo uwanjani.
Mchezo wa mpira upo wazi kwa kila mmoja kuona kile ambacho
mchezaji anakifanya iwapo atashindwa kufanya vizuri inamaanisha kwamba
hakujipanga na alikuwa hajui anahitaji nini.
Hakuna ruhusa ya kuzembea kutimiza majukumu kwa mchezaji akiwa
ndani ya uwanja pamoja na wakati huu ambapo amepewa program ya kufanya.
Kwa matokeo mazuri ambayo ni furaha ya timu na mashabiki lazima
kupanga mpango makini kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi ili kuona
wanapata kile wanachostahili.
Endapo ligi itareja tunaingia kwenye dakika za mwisho kumtafuta
bingwa mpya ambaye atatwaa taji lake msimu wa 2019/20 ni muhimu pia kulitambua
hilo.
Tayari timu nyingi zilikuwa zimecheza mechi nyingi za ligi na
ilikuwa ipo mzunguko wa pili ambapo timu nyingi zimebakiwa na mechi 11 na
nyingine 10 hivyo ni mua mchache umebaki.
Kwa mechi ambazo zimebaki ni mwendo wa hesabu ka kila timu kuona
itavuna nini iwapo itamaliza mechi zake zilizobaki kwa sasa.
Zipo ambazo hazina bahati kwamba hata ikitokea zikashinda mechi
zote haina uhakika wa kubaki kwene ligi hii ni hatari.
Changamoto ni lazima ziwepo lakini suluhisho pia ni muhimu
kutafutiwa hasa kwa muda huu ambao hauna presha kwenye mechi za ushindani.







0 COMMENTS:
Post a Comment