WANAFAMILIA wa Yanga ambao ni mabosi pia Kampuni ya GSM imesema kuwa iwapo kuna klabu ndani ya Bongo ama nje ya nchi itahitaji saini ya nahodha Papy Tshishimbi inapaswa isubiri mpaka mkataba umalizike.
Maneno hayo ni ujumbe kwa watani wao Simba ambao ilielezwa kuwa wanahitaji saini ya nyota huyo ili akaongeze makali ndani ya kikosi cha Simba.
Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya GSM Injinia Hersi Said amesema:"Kuhusu kapteni Tshishimbi yeye ni mchezaji muhimu na tumemalizana naye ambapo dili limekamilika na yeye mwenyewe amekubali kwa kusema 'dealdone'.
"Kwa wale ambao wanahitaji kuipata saini yake basi inawabidi wasubiri mpaka pale mkataba utakapoisha ili waweze kuipata saini yake ila kwa sasa atabaki ndani ya Yanga,".
Inaelezwa kuwa mkataba wa Tshishimbi ambao ulikuwa unameguka mwezi wa nane umeboreshwa kwenye upande wa maslahi jambo ambalo limemfanya akubali kusaini.
Mimi namshauri huyo Tshishimbi abaki tuu huko yanga, kwenda simba hakutamsaidia yeye wala yanga wala simba, sana sana makelele tuu. Amalizie mpira wake yanga, umri umemtupa mkono huyo
ReplyDeleteUnamshauri wewee kama nani, mikia wameshindwaaaa
DeleteKama mimi
ReplyDeleteWala Simba hawakuwa na haja naye Ila kwa sababu alitamka mkataba mnono ndio akawa anasingizia Simba wanamtaka Mara akihojiwa Mimi nikicheza na mkude, Dilunga na chama timu itakuwa moto
ReplyDeleteHivi mwenye blog hii hana habari tofauti na za Tshishimbi na bao la Morrison?
ReplyDeleteHuyo Tshishimbi ni uti wa mgongo kwa Yanga na ni maamuzi sahihi kubakia huko alipo kama ni kweli alitakiwa na Simba kwasababu angelijikuta anasugua bao tu. Angelikuwa huku kumnyangnya namba nani, Mkude, Chama, Kahata au nani?
ReplyDeleteBlog hii ya Yanga imemsaidia kupata mkataba Yanga. Angecheza wapi Simba??
ReplyDelete