UONGOZI wa Simba umesema kuwa Yanga walistahili kushinda mechi yao iliyochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa kutokana na kuwazidi mbinu.
Yanga iliwashinda Simba kwa kuifunga bao 1-0 bao lililofungwa na Bernard Morrison dakika ya 44.
Habari kutoka ndani ya Uongozi wa Simba zimeeleza kuwa walistahili kuchapwa kwenye mechi hiyo kwa kushindwa kufanya vizuri.
"Tulistahili kufungwa kwa kuwa hatukufanya vizuri na wapinzani wetu walipiga mpira mwingi na pasi za maana kuliko sisi, haikuwa kazi rahisi licha ya wachezaji kujituma.
"Wachezaji wao walikuwa wanagongana na walicheza kwa kujituma jambo ambalo liliwabeba ila hatukuwa na namna tuliamini tungerudisha bao ila haikuwa hivyo," alieleza kiongozi huyo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa alishindwa kuendelea kuutazama mpira baada ya kufungwa jambo lililomkosesha raha.
"Sikuwa Bongo nilitazama mpira nikiwa nje ya Bongo tulipofungwa hali haikuwa shwari kwangu," alisema.
Hii nayo ni habari? Mtu mmoja sio uongozi simba, labda kiongozi simba, maana sio tamko la kikao
ReplyDeleteHawajui hata viongozi ni nani manara kaajiliwa Simba wakimchoka anatimuliwa anaajiliwa mwingine
ReplyDeleteKwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa kuna kiongozi pale simba ambaye hawezi kitimuliwa? Maana wote ni waajiliwa kwa klabu hakuna ambaye hawezi kutotimuliwa iwe na wanachama aula
DeleteAchana nao,hao mbeleko fc hawajitambui
Deletehizi ni habari za kutunga ili kuuza gazeti hivo ni za kupuuza
ReplyDeleteElimu yenu ya kuungaunga hamjui tofauti ya mwajiliwa na kiongozi
ReplyDeleteMimi Nina mashaka na huyu mwandishi inawezekana tunamlaumu bure kumbe Ni empty kichwani
ReplyDeleteanaonekana empty kwa habari hii!
ReplyDeleteangeandika habari za kuisifia ssc wala usinge anddika haya,
lkn ukweli utabaki yanga ni mme wenu