TUNAZIDI
kuwa kwenye wakati mgumu kwa sasa kutokana na kila mmoja kuwa na hofu ya kusambaa kwa Virusi vya Corona
kitu ambacho kitaalamu kinapoteza uwezo wa asili wa kupambana kutafuta suluhisho.
Kwa sasa
bado janga kubwa la dunia ni kusambaa kwa Virusi vya Corona ambapo mgonjwa wa
kwanza kugundulika alitokea nchini China
ilikuwa Desemba,2019.
Kila mmoja
amekuwa akiripoti namna anavyotambua kuhusu Corona ila kinachotakiwa ni kuacha
kuwa na hofu na kuamini kwamba ugonjwa upo lazima tuchukue tahadhari.
Nyakati
ngumu pia huwa inakuwa vigumu kupata majibu sahihi iwapo kila mmoja atataharuki
kutafuta majibu anayoyataka ni lazima tutulie na kuendelea kuomba ili mambo
yapite salama.
Kwa wachezaji
ambao kazi yao kubwa ni kucheza kwa sasa wapo kwenye mapumziko ya lazima kwani
Ligi Kuu Bara nayo imesimamishwa na Serikali ili kuzuia maambukizi zaidi.
Kwa upande
wa wanafunzi tunaona kwamba shule zimefungwa ikiwa ni pamoja na vyuo lengo ni
moja kuzuia maambukizi zaidi kwani afya ni utajiri wa kwanza.
Mambo
yamekuwa tofauti kwa baadhi ya wazazi na walezi wameacha suala hili mikononi
mwa Serikali bila kujali afya za watoto.
Baadhi ya
wazazi wamekuwa wakiwaacha watoto kwenye mijumuiko isiyo ya lazima na wanafunzi
hao wanaendelea kucheza mpira ama kuwa kwenye mikusanyiko ya watu wengi jambo
ambalo linapaswa lichukuliwe tahadhari.
Katika hili
kila mmoja jukumu ni lake kuhakikisha anakuwa balozi mzuri kwa kulinda afya ya
mtoto pamoja na jamii nzima kiujumla kwa ajili ya tahadhari ya Virusi vya
Corona.
Tusisubiri
kila sehemu tukumbushwe na Serikali, gharama za matibabu ni kubwa muhimu kwa
sasa kuchukua tahadhari.
Wale ambao
wamekuwa wakijali na kuwapa elimu wanafunzi nawapongeza kwani sio wote hawajali
hapana wapo ambao wanajali lakini wachache wanaoacha hili lazima lidhibitiwe.
Kuwaruhusu
waendelee kucheza ni hatari iwapo itatokea maambukizi basi kasi ya kusambaa
itakuwa kubwa na gharama zake pia zitaongezeka.
Wachezaji
pia muda wa kuendelea kufanya mazoezi ya kujiimarisha ili kulinda kipaji ni
muhimu kwa kufuata program ambazo mmepewa na walimu wenu.
Pia kwa wale
ambao hawajapewa bado wanaweza kujipa mazoezi wenyewe wakiwa nyumbani kwani
bado wana muda wa kufanya mazoezi kabla ya ligi kurudi.
Iwapo
mchezaji atashidwa kujipa mazoezi yeye mwenyewe wakati ligi itakapoanza
atashindwa kuendelea pale alipoishia itamchukua muda mrefu kurudi kwenye ubora.
Kinachotakiwa
ni kuchukua tahadhari na kufanya mazoezi pamoja na kuzingatia maelekezo ambayo
mmepewa na makocha.
Kila mmoja
akichukua tahadhari itasaidia kupunguza maumivu pale maambukizi yatakapotokea
na kila mmoja atakuwa katika usalama.
Elimu
inabidi iendelee kutolewa kuhusu janga hili ili kila mmoja atambue vizuri kwani
inaonekana kuna baadhi ya maeneo hasa ya kule vijijini bado hawajapata taarifa
sahihi.
Wakati huu
kwa wale ambao watakuwa wanatoka mjini na kuelekea vijijini wawe mabalozi
wazuri katika hili na wafanye jitihada kuwapa taarifa sahihi kwa kile abacho
wanauhakika nacho ikiwa ni ngumu basi wazungumze na wataalamu wa afya.
Kwa wale
wataalamu wa afya wasichoke kuzungumza na watu wao na kuwapa tahadhari pia
kwani wengi bado wanadhani ni kitu cha kawaida jambo ambalo linawafaya
wasichukue tahadhari.
Mungu
atufanyie wepesi katika hili suala ambalo lilianza kama utani lakini kwa sasa
limekuwa ni janga.
Wachezaji
bado nitazidi kuwaambia kwamba wasisahau kufuata maelekezo ambayo wamepewa na
makocha wao kwa kuendelea kulinda vipaji vyao kwa kufanya mazoezi.
Afya yao pia
ni suala la kuzingatia kwa kuchukua tahadhari jambo litakalowafanya wawe salama
katika wakati huu ambao nina amini ni wa mpito.
Ni wakati
ambao kila mmoja anatakiwa kuwa makini na kufuata tahadhari ya kile ambacho
anaambiwa ili awe salama.








0 COMMENTS:
Post a Comment