DAVID Molinga, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kuna umuhimu wa mashabiki wakatambua thamani ya wachezaji wakiwa ndani ya uwanja licha ya kufanya makosa madogo wanapokuwa uwanjani kwa kushindwa kupata matokeo.
Molinga amekuwa akikutana na wakati mgumu kwa kuzomewa na mashabiki ambapo kwenye mchezo waliolazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC, mashabiki waliwajia juu wachezaji ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wao mwili jumba, Yikpe Gnamien.
Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC uliopigwa Uwanja wa Taifa, Molinga akitokea benchi kuchukua nafasi ya Balama Mapinduzi alitupia mabao mawili na kuweka usawa wakati Yanga ikilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.
Molinga amesema:"Ninawapenda mashabiki kwa kuwa wanakuwa nasi bega kwa bega ila wanapaswa watambue kuwa hata sisi pia huwa tunaumia pale tunapokosa matokeo hivyo tunapambana kufanya kila kitu kiwe sawa."
Kibindoni Molinga ametupia jumla ya mabao 10 akiwa kinara kwa watupiaji ndani ya Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael.
Leo itakuwa na kazi Uwanja wa Taifa kumenyana na Ndanda FC ya Mtwara iliyo chini ya Meja Msataafu, Abdul Mingange.

Almuradi baada ya mabao kumi aliyotapachika na atayopachika akae tayari kutimiluwa kama walivokuwa wanatamka viongozi na mashabiki kumuandama Bila ya rehema
ReplyDelete