June 27, 2020



KOCHA Mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool, Jurgen Klopp inaripotiwa kuwa anahitaji kupata saini ya nyota wa Napoli, beki Kalidou Koulibaly.
Kichapo cha Manchester City siku ya Alhamis cha mabao 2-1 kutoka kwa Chelsea, Uwanja wa Stamford Bridge kimeipa nafasi Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kupita miaka 30 jambo linalomfanya Klopp afikirie kuboresha zaidi kikosi chake.
Klopp anatazama namna ya kuongeza makali kwenye kikosi chake ambapo kwa sasa anaye Van Dijk ambaye ndiye tegemeo ndani ya kikosi hicho kwa upande wa ulinzi akiwa amehusika kwenye mabao 21 ndani ya Ligi Kuu England msimu huu.
Inatajwa kuwa Koulibaly anawaniwa vikali na Chelsea, Manchester United   ambao wanamhitaji beki huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya Napoli.
Raia huyo wa Senegal mwenye miaka 29  pia anahusishwa kuwindwa na Manchester City ambayo inanolewa na Pep Guardiola huku thamani yake ikitajwa kuwa ni paundi milioni 90.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic