June 4, 2020


IMEELEZWA kuwa, Kocha Mkuu wa Azam FC, Arstica Cioaba alilazimika kudanganya kuwa ni dereva wa lori ili kuvuka mipaka ya Romania, Hungary na kuibukia Ujerumani ambako alipata ndege kurejea Tanzania.

Cioaba raia wa Romania alifanya hivyo kwa kuwa nchi yake haijafungua mipaka hali kadhalika Hungary na Ujerumani pekee ndio wameruhusu ndege kupaa na kutua.

Kocha huyo alipanda lori akiwa na kocha wa makipa na Msaidizi wake na walieleza kuwa wao ni madereva wasaidizi pia mafundi kwa kuwa sheria ya nchi hizo inaruhusu malori tu kusafiri na si abiria.


Tayari Cioaba ametua nchini na kuanza kukinoa kikosi chake ambacho kinajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC utakaopigwa Juni 14, Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic