June 4, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa itakuwa ngumu kwa sasa kumpata kiungo wao Sharaf Shiboub raia wa Sudan kutokana na mipaka ya nchi yao kufungwa.

Shiboub aliibukia Sudan baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo Machi 17 na kwa sasa tayari Serikali imeruhusu shughuli za michezo kuanza kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi  ya Virusi vya Corona imepungua.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema:"Ni ngumu kumpata Shiboub kwa sasa kwani sheria za nchini kwao ni ngumu na mpaka sasa mipaka haijafunguliwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

"Bado jitihada zinaendelea ila kwa wakati huu hatutakuwa naye kwani mambo bado hayajawa shwari kwake kurejea,"

Simba ilianza mazoezi Mei 27 ambapo wachezaji wanne ambao walishasepa nchini tayari wawili wameungana na wenzao mazoezini ambao ni Meddie Kagere wa Rwanda na Francis Kahata wa Kenya. Clatous Chama wa Zambia anatarajiwa kurejea muda wowote kuanzia sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic