IMERIPOTIWA kuwa Manchester City haipo tayari kumuachia nyota wake Raheem Sterling ambaye anawindwa na wapinzani wao wakubwa Manchester United wakiitaka saini yake.
Mkataba wa mshambuliaji huyo ndani ya City unatarajia kumeguka mwaka 2023 na sababu kubwa inayowapa nguvu United kumpata ni kufungiwa na UEFA miaka miwili kutoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Nyota huyo alitua ndani ya City msimu wa 2015 akitokea Klabu ya Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp ambapo akiwa huko msimu wa 2012/15 alicheza mechi 95 na kufunga mabao 18.
City imesema kuwa itaendelea kusalia na nyota huyo ambaye amecheza jumla ya mechi 155 na kufunga mabao 59 ndani ya City.
0 COMMENTS:
Post a Comment