June 4, 2020


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael tayari ameshatumiwa tiketi yake anachosubiri kwa sasa ni kurejea nchini kuanza majukumu yake.

Eymael alisepa nchini na kuibukia Ubelgiji, baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona Machi 17.

Awali ilielezwa kuwa hakutumiwa tiketi na viongozi wa Yanga jambo ambalo lilikuwa linampasua kichwa akifikiria kufanya kazi yake akiwa mbali na timu ambayo imeshaanza maandalizi ya mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho.

"Tayari ameshatumiwa tiketi na kila kitu juu yake kinakwenda sawa wakati wowote kuanzia sasa anaweza kurejea inaweza kuwa Juni sita ama saba kulingana na namna hali itakavyokuwa," ilieleza taarifa hiyo.

Yanga kwa sasa ipo chini ya Kocha Msaidizi, Charles Mkwassa mchezo wake wa kwanza itakuwa ni Juni 13 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic