June 27, 2020





Na Saleh Ally
 UMESIKIA mengi kuhusiana na kiungo mwenye kasi wa Yanga, Bernard Morrison kutoka Ghana. Kwamba kuna fedha dola 5,000 alipelekewa na wakala aliyemuambia kwamba zimetolewa na viongozi wa Simba.

Hii ilisikika katika sauti yake iliyovuja mitandaoni na ikaelezwa alichukua. Lakini kumekuwa na mengi yanazungumzwa kuhusiana na mkataba wake mpya kama kweli upo ni ule wa miezi sita au ana mpya wa miaka miwili!

Ili kupata majibu sahihi ya hilo, ni Morrison pekee ndiye anaweza kutoa kupitia SALEHJEMBE BLOG. Tumefanikiwa kumpata na kufanya naye mahojiano maalum.


SALEHJEMBE: Kipi hasa ukweli kuhusu mkataba wako na Yanga, miezi sita au una miaka miwili?

Morrison: Nianze kuwashukuru mashabiki kutokana na walivyonionyesha mapenzi katika mechi ya Azam wakati naingia. KUhusiana na mkataba nimesikia mengi sana, kwamba naondoka, sitaki kuichezea Yanga, mambo ni tofauti sana.



SALEHJEMBE: Hayo tofauti waeleze wayajue…
Morrison: Sijawahi kuleta ulalamishi, kusikia sitaki kuichezea Yanga si sahihi. Mfano wakati nilipotua hapa nchini, niliichezea Yanga mechi mbili bila ya kuwa nimeingia mkataba nao, nilifanya hivyo kuwaonyesha Imani na upendo. Nilipozungumza na kocha (Eymael), akaniambia niuamini ungozi, nimuamini Injinia Hersi, kabla ya kusaini mkataba, nikaanza kuitumikia timu.

SALEHJEMBE:Baadaye ikawaje?
Morrison: Nikakubali, nikasafiri na timu kwenda Singida na nikacheza, tukarudi Dar es Salaam, nikacheza n ahata sikuwa na mkataba. Kwangu ilikuwa ni mapenzi makubwa hadi hapo baadaye tulipokubaliana na kusaini mkataba wa miezi sita. Lakini nashangazwa na hizi habari kwamba sasa sitaki kuichezea Yanga, si kweli hata kidogo.

SALEHJEMBE:Mkataba wako hasa ni muda gani na unaisha lini?
Morrison: Mkataba wangu na Yanga ni miezi zita, unaisha mwishoni mwa mwezi ujao. Kikubwa mashabiki wajue nitaitumikia Yanga kwa juhudi na nguvu zote bila ya kuchoka na ninasema hivi kwa kuwa mashabiki wana haki ya kujua kinachoendelea, ndio maana nimekuwa tayari kuzungumza.

SALEHJEMBE: Mpango wako kuongeza mkataba ukoje, maana huu umeisha?
Morrison: Kuna mengi yanaendelea, nasubiri tuzungumze kuhusiana na mkataba mpya lakini ukweli sina furaha kwa sasa licha ya kwamba niliwaamini sana viongozi. Kwa mashabiki, sina shida nao, nataka kuwatumikia hadi mwisho.



SALEHJEMBE: Kwanini hauna furaha?
Morrison: Kuhusiana na ile clip iliyosambaa mitandaoni, kwamba nilichukua fedha dola 5,000. Nilipokea fedha kutoka kwa wakala ambaye alisema zile fedha ni sehemu ya ushawishi nisaini Simba. Kila mtu anahitaji fedha, hakikuwa kitu cha lazima, nikachukua.

SALEHJEMBE: Lakini ajenti alikuwa ni fedha kutoka Simba? Ulizungumza nao Simba?
Morrison: Ndio alisema, lakini mimi sijawahi kuzungumza na mtu yoyote kutokea Simba wala simjui yoyote isipokuwa yule mmiliki wa Simba,Mo (Dewji) ambaye ninaamini kila mtu anamfahamu na kamwe pia sijawahi kuzungumza naye.
SALEHJEMBE: Huyu wakala ni nani?
Morrison: Ni mtu kutokea Ghana na alipokuja kwangu niliona ni kama ndugu yangu.

SALEHJEMBE: Ulisema kakuambia fedha zinatokea kwa Rais wa Simba?
Morrison: Ndio alinieleza vile lakini sasa sijui kama ni kweli au la, unajaua wakala akiwa kazini atafanya kila analoweza na ikifanikiwa baadaye utatakiwa kumlipa na hapa unaona zile fedha zake zingerudi kwake tena. Sina uhakika alichokuwa amenuia hasa.


SALEHJEMBE: Ulipopokea fedha hizo, ulizungumza na yoyote kumueleza kwamba ulipokea fedha kutoka Simba?
Morrison: Ndio, nilifanya hivyo mara moja, nilizungumza naye ambaye kweli ndiye nilikuwa mtu ninamuamini kuliko mwingine yoyote katika klabu. Yeye ndiye alifanya hata nicheze Yanga mechi mbili bila ya kuwa hata na mkataba


SALEHJEMBE:Ulimfuata, au mliwasiliana vipi?
Morrison: Nilirekodi voice note nikaituma kwake, nikamueleza kuwa kuna mtu kaja, kanipa fedha ni wakala kutoka Ghana na anasema zimetokea Simba. Basi akaniambia nimesikia kaka, nitakupigia na tuongee. Nikawa nasubiri lakini hakunipigia tena kwa kama miezi mitatu au minne, hakuweza kuzungumza tena na mimi kuhusiana na hizo fedha. Nikaona basi aliona ni kitu cha kawaida sana, hakuwa amejali sana, nami nikaendelea na mambo yangu.


SALEHJEMBE:Ikawaje baada ya hapo?
Morrison: Kiukweli ninaiheshimu sana Yanga ndio maana nikaona kumpigia na kumueleza. Baada ya pale, nikaanza kuona ile sauti niliyomtumia kumuelezea kilichopo kuhusiana na yule wakala aliyesema fedha kutoka Simba inaanza kusambaa mitandaoni, nilichanganyikiwa, sikupenda na sikuelewa.


SALEHJEMBE: Hapo tatizo ni lipi, huenda alitaka watu waelewe kinachoendelea?
Morrison: Hii ni siri ya ndani ya klabu, siri baina yetu na lengo langu la kutoa taarifa ili watu wa klabu waelewe. Sikuzungumza kwenye vyombo vya habari au kuweka kwenye mitandao ya kijamii. Mtu anaweza akasikia vile na asielewe, mtu anaweza hata kukua kwa kuchukua fedha kutoka Simba.


SALEHJEMBE: Una hofu watu wanaweza kukudhuru?
Morrison: Ndio, mimi ni binadamu, shabiki anaweza kukasirishwa kutokana na wewe kuchukua fedha kutoka Simba, akakudhuru au kukua. Kiukweli kiongozi hakujali kuhusiana nami, ajabu atataka niendelee kufanya kazi na klabu kwa furaha?


SALEHJEMBE: Umewasiliana naye?
Morrison: Hapana, nilikasirika sana na anajua ninajua yeye ndiye alisambaza ile sauti. Kiukweli sijui kama ninaweza kujadili naye hili suala, kwamba vipi tuzungumze halafu usambaze maana nina hofu, chochote nitakachosema tena kinaweza kusambaa mitandaoni kwa mara nyingine, nitaendelea kuwa katika hali ya hofu.


SALEHJEMBE: Nikisema sasa wewe na Injinia Hersi hamuelewani?
Morrison: Hapana, si kama hatuelewani lakini kunakuwa na mipaka ya baadhi ya mambo. Kikazi mimi ni mtu wa weledi, nitafanya kazi yangu kwa juhudi kubwa kwa kuwa najua naitumikia Yanga na si vingine. Lakini kuna vitu nitapunguza kwake sababu Imani yangu imeshuka kwake kutokana na alichonifanyia ambacho si kitu cha mtu anayefuata taratibu.


SALEHJEMBE: Zile fedha dola 5,000 kutoka kwa wakala, nilisikia zinatakiwa kurudi, umefanyaje? Kama unazo, unaweza kuniambia umetumia kwenye mambo gani?
Morrison:

SALEHJEMBE:Zile fedha….

INAENDELEA HATUA YA PILI KATIKA BLOG HII....


7 COMMENTS:

  1. Wewe mwandishi unakuja mipaka yako ya uandishi.Unapoweka title fedha za Simba una uhakika?Simba wameshakanusha! Nini azma yako katika kuendeleza hili tukio?Umewahoji Simba?Ethics za journalism ni kuwa nä habari za pande zote mbili ili kubance stori. Umemhoji Injinia Said Hersi?

    ReplyDelete
  2. Ila wewe mwandishi kwa hakika ni mchochezi na unachangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibu soka la Tanzania. Hii yote ili upate hela tu. Ila malipo ni hapa hapa duniani.

    ReplyDelete
  3. jembe ww ni mchochezi unatumika na simba kuivuruga yanga,umemponza morrison kapewa adhabu na timu yake sababu yako.ww ni mweledi kaka siyo kanjanja

    ReplyDelete
  4. iyo inaitwa ukichimama nchale ukimbia nchale yanga poleni sana, tatizo viongozi wenu wanaleta mambo ya bongo movie kwenye mpira au walijuwa morisoni ni kama mrisho ngasa atacheza yanga kwa mapenzi, morisoni hana Imani na uwongozi wa yanga so picha inaenda kukamilika time yeyote pia tff waje na nyundo kubwa kwa yanga kwa nni jamaa amecheza ligi pasipo kuwa na leseni 😂😂😂

    ReplyDelete
  5. Saleh Jembe umesomea wapi uandishi wa habari maana inakuwa kama unamlazimisha Morrison amechukua dola 5,000/-toka kwa kiongozi wa klabu ya Simba na Morisson ana kusisitizia amechukua pesa toka kwa wakala wake aliyempeleka Yanga.Morrison hana kosa la kuchukua hiyo pesa wala wakala wake hajafanya kosa kumpatia hiyo pesa ya Chai.Morrison na wakala hawafungwi na sheria sababu wanajua walifanya hivyo wakijua wana mkataba wa miezi sita ambayo inamruhusu mchezaji kufanya mazungumzo na klabu nyingine.Kama Morisson amechukua hiyo pesa na baadaye akaghairi kuendelea na mazungumzo kama alivyosema anaenda kutafakari basi amrejeshee pesa yake wakala.Vinginevyo biashara yao ni moja.Lakini hata hivyo bado kuna utata na kauli za Morrison kwa nini anasisitiza mkataba wake unaisha mwezi ujao? Yanga wanasema amesaini mkataba wa miaka miwili lkn kuna vipengele vya kisheria ambavyo ni siri ya Morrison na Injinia Hersi kama matakwa ndani ya mkataba huo yametimizwa? Na kama hayajatimizwa basi mkataba ni batili.Saleh Jembe mwangalie kwa jicho la tatu Morrison na wakala wake vinginevyo mambo yanaweza yakawa tofauti na tunavyo fikiria.kumbukeni biashara ya Okwi na Yanga.Sakata la madai ya kina Obrey Chirwa, Hamis Tambwe,Lwandamina,Pondamali na wengineo wanaoidai Yanga pengine yanowafanya wachezaji wapya wanao taka kujisajili kusita na figisu-figisu za viongozi wa Yanga.Tuwe wakweli uendeshaji wa klabu ya Yanga umejaa ubabaishaji na viongozi kwa nini hawataki kubadilika? Nawapongenza wanachama wa Simba kwa kuamua kutogeuka jiwe na kuendelea na mabadiliko walioyaumua licha ya misukosuko wanayopitia na kuwapotezea kina kilomoni.

    ReplyDelete
  6. Mimi bado sielewi, iliwezekanaje mchezaji acheze mechi 2 bila kuwa na mkataba? Ina maana Mchezaji anaruhusiwa kucheza kwa barua au? Yaani iliwezekanaje? Na hizo timu zilizocheza na Yanga Morrison akiwemo wakilalamika kuna usalama kweli? Mwandishi naona peleleza vizuri, kama aliyoyasema Morrison ni ya kweli basi pale TFF kuna mkataba feki wa Morrison. Kwa sababu Morrison anasema aliingia mkataba na yanga wa miezi 6 ambao unaisha July 2020. Uongozi wa GSM unasema waliingia mkataba wa miezi 6 baadae wakaongeza wa miaka miwili. Lakini taarifa iliyotolewa na yanga inasema mwezi January walimsainisha mkataba wa miaka 2 unaokoma July 2022. Hapa kuna mkanganyiko maana kuna upande unakubaliana na Morison kwa kiasi fulani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic