June 25, 2020


BAADA ya Klabu ya Yanga kumalizana na beki wa kushoto wa Rayon Sports ya Rwanda, Eric Rutanga, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kudai kuwa Yanga wamepata mtu wa kazi katika eneo la ulinzi.

Mmoja wa viongozi wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Rayon Sports, Jean Luc, alisema kuwa Rutanga ni mmoja wa wachezaji wazuri akicheza kama beki wa kushoto kwani mbali na uwezo wake wa kupanda kushambulia na kurudi kukaba, pia ana uwezo mkubwa wa kupiga faulo.

Jean Luc alisema kuwa Yanga wamepata mchezaji mzuri katika eneo la ulinzi kwa kumsajili Rutanga, kwani ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa ndiyo maana amekuwa hakosekani katika kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi kutokana na uwezo wake.

“Rutanga ni mchezaji mzuri sana, anaweza kwenda kushambulia na akarudi kwenye nafasi yake na kusaidia kukaba, lakini ukiacha hivyo, anaweza sana kupiga mipira iliyokufa kama kona na faulo, Yanga wamepata mchezaji sahihi kusema ukweli,” alisema Jean Luc.

Meneja wa Rutanga, Harve Tra Bi alithibitisha kuwa mchezaji huyo amekubaliana mkataba wa miaka miwili wa kukipiga Jangwani. Mchezaji huyo alitumiwa mkataba kwa barua pepe kutokana na mipaka ya Rwanda kuendelea kufungwa kutokana na Corona.

7 COMMENTS:

  1. Kila siku wao hao yanga wanamalizana na wachezaji sasa watakuwa 100 wamefika na usajiri bado hadi ukianza usajiri watakuwa wachezaji 200

    ReplyDelete
    Replies
    1. Next time watakuja na habari nyingine ambayo itakuwa ni kinyume na hii maana kwa hawa jamaa kwa kupika habari nimewavulia kofia.Wanastahili kuitwa Mabeberu wa kutunga habari

      Delete
  2. Mtapata kila Aina ya mchezaji mazuri lakini kwa msimu ijayo ya karibu kwa Simba hii chini ya uongozi wa Moo, ubingwa muusahau

    ReplyDelete
  3. Mbona waandishi hawaendi msimbazi kuulizia kuhusu uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ambapo Serikali ineamuru ufanyike....lakini kutwa kutafuta habari za Yanga???Watu wamechoka kutwa habari za Yanga zinapoteza mvuto na ladha sasa kama hamlijui hili mlijue sasa...nyie tafuteni habari za Simba sasa!

    ReplyDelete
  4. Wameambiwa wafanye uchaguzi na muda wamepewa sasa inakuwa habari kweli?Ungengojea Oktoba ulete hizo theories zako. Unachosha na hadithi zako za njama kila siku bila ushahidi. Grow up.

    ReplyDelete
  5. Naona wananchi hawana mpya, zaidi ya kulalamika. Molinga kakataa fedha zenu.

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli Yanga haitokamatika kwasababu nyota waliokwisha nao ni kweli zaidi ya Mia mbali na wazawa lakini kutokana na gongonje walivo wasitaraji kuona mwanga. Huyu kafika huyo anatimuliwa kwakuzomewa na kusimangwa. Uwapi utulivu na morali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic