July 31, 2020

BAKARI Mwamnyeto, beki chipukizi anayekipiga ndani ya Coastal Union inaelezwa kuwa ameshatua Dar akitokea Tanga kwa ajili ya kukamilisha dili la kujiunga na Yanga.

Habari zinaeleza kuwa wakati wowote kuanzia leo nyota huyo atamalizana na Yanga ambao wamepania kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21.

"Mwamnyeto ameshatua ndani ya Bongo huenda akamalizana na Yanga muda wowote kuanzia sasa,ila kinachochelewesha ni dau tu la usajili wake.

"Anahitaji apewe milion 70, mabosi wanataka waanze na milioni 30 kisha zilizobaki watammalizia baadaye, ninaamini hawatazembea kwani Azam FC nao wanahitaji saini yake hivyo hawatakubali yatokee kama yale ya Awesu," ilieleza taarifa hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawana presha na usajili wa msimu huu watafanya mambo makubwa kwa kuzingatia utaalamu wa kazi.

1 COMMENTS:

  1. NENDA SIMBA AU AZAM ILI KUKIDHI HAJA YA SALEH JEMBE./ SALEH ALLY. ANAZUGA UNAENDA YANGA ILI SIMBA AU AZAM WAKUSAJILI.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic