MEDDIE Kagere,
mshambuliaji namba moja ndani ya Simba hatimaye guu lake limeibuka Uwanja wa
Taifa baada ya kuyeyusha dakika zaidi ya 354 bila kufunga.
Mara ya mwisho Kagere
kucheka na nyavu ilikuwa ni Machi 11 aliwatungua Singida United kwenye mchezo
wa Ligi Kuu Bara wakati Simba ikishinda mabao 8-0, Uwanja wa Uhuru yeye
alitupia mabao manne na kufikisha jumla ya mabao 19.
Baada ya hapo hakukuwa na mechi za ushindani tangu Machi 17 kutokana na janga la Corona ila mambo yalipotulia Serikali iliruhusu masuala ya michezo kuendelea Juni Mosi, Kagere alishindwa kufurukuta kwenye mechi tano mfululizo bila kufunga wala kutoa pasi ya bao ndani ya uwanja.

Juni 14 alitumia dakika 90 mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa na
Simba ilitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1.
Juni 17 alizimega dakika 28 wakati Simba ikishinda mabao 3-0 mbele ya Mwadui FC, Juni 28 alitumia dakika 90 mbele ya Tanzania Prisons kwenye sare ya bila kufungana Uwanja wa Sokoine.
Julai 5 alitumia dakika 21 mbele ya Ndanda FC wakati
Simba ikikubali sare ya bila kufungana, Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Julai 8
alizimega dakika 90 mbele ya Namungo na kufanya atumie dakika 319 hizi zote
zilikuwa ni za ligi.
Julai 12 mbele ya Yanga mchezo wa FA alitumia dakika 17 wakati Simba ikishinda mabao 4-1 Uwanja wa Taifa na akaibukia mbele ya Mbao FC dakika ya 35 wakati Simba ikinyooshwa mabao 3-2 na Mbao FC akifunga bao dakika ya 35 kwa mkwaju wa penalti na kufanya guu lake liibuke baada ya kupita zaidi ya dakika 354 akifkisha mabao 20 ndani ya ligi.

0 COMMENTS:
Post a Comment