WAKIWA tayari wana taji
lao kibindoni kwa mara ya tatu mfululizo, Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven
Vandenbroeck imeweka rekodi ya kushinda mechi nyingi za ugenini kwa msimu wa
2019/20 ikifuatiwa na Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael.
.
Simba imecheza mechi 17
ambazo ni dakika 1,530 ugenini sawa na Yanga. Simba imeshinda mechi 12 na
kulazimisha sare tatu huku ikipoteza mechi mbili ugenini ambayo ni dhidi ya
Mwadui FC na JKT Tanzania zote ilifungwa bao mojamoja na kujikusanyia pointi
39.
Yanga imeshinda mechi nane na sare saba huku ikipoteza mechi mbili ugenini ikiwa ni mbele ya Azam FC na KMC zote ilichapwa bao mojamoja na imejikusanyia pointi 31.
Singida United iliyokata tiketi ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao imetia fora kwa kushinda mechi mbili ugenini mbele ya Mbeya City na Ruvu Shooting huku ikipoteza mechi 13 na sare nne na kujikusanyia pointi 10.

0 COMMENTS:
Post a Comment