July 28, 2020




Anaandika Seleman Matola


AGOSTI 2 Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga inatarajiwa kuchezwa fainali ya Kombe la Shirikisho.Mchezo huo ni mkubwa na una heshima ndani ya Tanzania.

Ukweli ni kwamba waandaaji wa mashindano hayo wamekuja na kitu cha kipekee kuanzia ushindani ulivyo mwanzo pamoja na kila timu kupambana kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Katika hilo ninapenda kuwapa pongezi siku zote mashindano yamekuwa na mvuto wa kipekee huku kila timu ikiwa na nafasi ya kuibuka na ubingwa ikiwa itajipanga.

Ni timu nyingi ambazo zinakusanywa kwa kuwa inakusanya timu za madaraja yote kuanzia Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili mpaka Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hapa nadhani unaona namna inavyokuwa na mvuto huku kila timu ikisaka ushindi kwenye mechi zake zote ili kufikia hatua ambayo wanahitaji.

Huku kila mchezo ni fainali kwani ukipigwa mchezo mmoja mwisho wa safari unawadia kwako na ndivyo ilivyokuwa kwa msimu huu wa mwaka 2019/20.

Yote kwa yote tumeshuhudia namna ilvyokuwa hatua kwa hatua mpaka kwenye hatua ile ambayo ilikuwa ina mvuto wa kipekee hatua ya robo fainali kisha nusu fainali na sasa ni fainali.

Zilizotinga fainali ni Simba na Namungo ambapo kwenye timu hizi mbili anakwenda kutafutwa bingwa wa Kombe la Shirikisho ambaye ataibuka kidedea tena nje ya Dar es Salaam.

Nina amini kuwa utakuwa mchezo mkubwa na wenye ushindani kwani kila timu inahitaji kupata ushindi ili kubeba taji kwani ndiyo malengo ya timu ambayo imetinga hatua ya fainali.

Sasa kinachonileta hapa leo nahitaji kuweka kwenye jamvi ni namna maandalizi yalivyo hasa kwenye fainali yenyewe inavyokuwa na inakokwenda kuchezwa.

Unajua kuna mambo mengine tunapaswa tutazame namna timu zinavyopambana kufikia mafanikio pamoja na kule ambako zinapelekwa kufanyia mashindano.

Haina maana kwamba Sumbawanga ni mbali ama hapafai hapana najua ni falsafa katika kuupeleka mpira kila kona ya Tanzania ila kuna mambo ya muhimu waandaaji wa mashindano haya wanapaswa wayatazame.

Unapoamua kupeleka fainali tena ya mashindano makubwa kama FA nje ya Dar es Salaam na kwenye mkoa ambao bado hakuna timu inayoshiriki Ligi Kuu Bara hii naona bado haijakaa sawa.

Msimu uliopita wakati nipo Lipuli nilifika na timu hatua ya fainali na ikachezwa huko Lindi, Ilulu haikuwa mbaya lakini ilikuwa na maumivu mengi.

Achana na kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Azam FC ninazungumzia mazingira ya Ilulu yalivyo hayakuwa rafiki kwa timu yangu pamoja na mimi kukaa huko hasa kwa upande wa maradhi na chakula.

Ilikuwa ni ngumu kwa timu kukaa sehemu moja kilichotakiwa kufanyika huko ni kuwagawa wachezaji kwa mafungumafungu ili waweze kukaa huko wakati wa maandalizi.

Pia upande wa miundombinu bado mambo mengi yanakuwa hayaleti picha nzuri zaidi ya kufanya mazingira kuwa magumu kwa wachezaji wote.

Tazama namna ambavyo gharama zilitumika kukikarabati kiwanja cha Ilulu kwa ajili ya fainali ya siku moja nini kimetokea kwa sasa? Hakuna timu ambayo inatumia kiwanja kile baada ya fainali.

Wakati huu ninaona maandalizi yameanza kukikarabati kiwanja kile cha Nelson Mandela ni jambo jema lakini cha msingi kujiuliza baada ya fainali kuisha ni kipi kitaendelea kwenye uwanja huo?

Itapendeza ikiwa waandaaji wataamua kuweka usawa katika maandalizi ya fainali ya Kombe la Shirikisho hasa kwa kuwa na sehemu moja ambayo itakuwa inajulikana na kila mchezaji tangu mwanzo wa mashindano.

Unajua haya mashindano yana hadhi ya kimataifa na mshindi pia anapata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa ya kimataifa hivyo itapendeza maboresho katika sehemu ya kuchezea fainali.

Bado nina amini kuwa Sumbawanga kutakuwa na tatizo la malazi kwa timu pamoja na viongozi hivyo mazingira yanaweza kuwa sawa na kule Ilulu hivyo ni muhimu kutazama upya katika kuandaa uwanja wa kuchezea fainali.

Sikatai kucheza Sumbawanga, hata ingepelekwa Njombe sawa hakuna tatizo lakini cha msingi ni kuangalia hadhi ya mashindano pamoja na gharama za maandalizi ya uwanja kwa wakati mmoja.

Labda kwa mfano tuseme  gharama za maboresho ya uwanja zingepelekwa pale Tanga Mkwakwani huenda ingepunguza kelele kwamba Mkwakwani hakuna uwanja mzuri.

Na ingesaidia pia kuongeza idadi ya viwanja bora ndani ya ligi msimu ujao kwa kuwa kuna timu za Ligi Daraja la Kwanza pamoja na Ligi Kuu zingeendelea kuutumia uwanja huo.

Ninadhani ingependeza tukifuata mfano wa FA ya Ulaya kule wenzentu wanachezea fainali pale Wembeley pana faida na ushindani unakuwa mkubwa huku wachezaji wakiweka alama kwamba wamewahi kucheza ndani ya uwanja mzuri duniani.

Kwa Tanzania ingekuwa inachezwa pale Uwanja wa Taifa ingependeza zaidi na kila mchezaji angekuwa anatambua kwamba anakwenda kucheza Uwanja wa Taifa.

Ujue kucheza Uwanja wa Taifa ni CV kuna wachezaji wengine wanaskia tu hawajawahi kucheza pale, nina amini kwamba katika hili wakati ujao itafanyiwa maboresho.

8 COMMENTS:

  1. You are absolutely right about that coach. Ina make more sense kama final ingekuwa Taifa kutokana na sababu ulizozitaja. Pia kwa kuongezea mshindi anaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa, huko wanakokwenda kupambana viwanja vina hadhi ya kimataifa, sasa kwa nini badala ya kuwandaa wachezaji wetu kwa kile wanachokwenda kukutana nacho, sisi tunang'ang'ania mambo yanayoturudisha nyuma ki soka.? Kama nia ni kupeleka fainal mikoani basi ushauri wangu kwa TFF ungekuwa hivi,
    Moja ya masharti ya kupeleka fainal mkoa husika lazima mkoa huo uwe na timu kwenye ligi kuu. Pili ni kwamba pindi tu wanapotangaza mkoa ambao fainal itachezwa, maandalizi au ukarabati wa uwanja husika yanatakiwa yaanze immediately ili wakati mashindano hayo yakiendelea na maboresho ya uwanja huo nayo yatakuwa yakiendelea, by the time mashindano yanafikia hatua ya final na uwanja huo uwe tayari kukabiliana na mchezo huo wa fainal, hayo ndio maoni yangu. I hope TFF italichukuliwa jambo hili seriuosly.

    ReplyDelete
  2. Nakuunga mkono Matola kocha wa kila mafanikio Mia kwa mia

    ReplyDelete
  3. Mtoa mada na wachangiaji, nawaunga mkono katika hili, kiuhalisia katika kukuza kiwango Cha soka swala la viwanja nalo linahusika Sana, Mm naona zaidi ya hayo Ni vizuri kufanya maboresho kwa viwanja vya timu zote za ligi ili viwe ktk standard na iwe Ni kwa mda wote.
    Uwekwe utaratibu wa kudumu kila uwanja unaotumiwa ligi kuu kufanyiwa maintenance na hii iwe ni wakati wote, ila tu wakati wa mashindano uboreshwe zaidi na itakuwa rahisi Sana Kama Hilo litazingatiwa. Kwa kufanikisha hili Ni vema kila chama Cha soka ktk mkoa wenye timu ya ligi kuu kwa kushirikiana na wamiliki wa viwanja na wadau wa mpira waweke miundombinu ya kudumu ya maintenance ya viwanja (haswa pitch) kwa mf. kuwa na Mfumo wa kudumu na wa kisasa wa maji katika kila uwanja kwa kunyunyizwa ktk pitch inapohitajika haswa msimu wa ukame/ kiangazi, mashine ya kukatia nyasi za kwenye pitch n.k. Ili uwanja wowote ukihitajika kutumika ktk fainali ya ASFC itasaidia hata waandaaji wa fainali hizi kupata wepesi na kazi yao itakuwa ndogo sana kwani watafanya marekebisho madogo madogo. Hili linawezekana ikiwa Tff, serikali kupitia wizara husika na wadau wataamua.

    Ili kukuza mpira, maendeleo ya mpira lazima yawe bega kwa bega na uboreshaji viwanja. Mfano Ni nchi zilizopiga hatua viwanja vyao vingi Ni vizuri hata Kama wana viwanja vibovu vipo ila Ni vichache tofauti na sisi viwanja vizuri vichache na vingi vibovu.

    ReplyDelete
  4. Kocha wa yanga ameongelea viwanja vibovu watu wanamshikia bango kuhusu ubaguzi haya mambo ya kuruhusu viwanja vibovu kisa wasikose kura za wajumbe hayatasaidia mpira wa Tanzania

    ReplyDelete
  5. Kwa hiyo we ulitaka watu wakae kimya kuhusu kauli zake za kibaguzi embu tuacheni ushabiki wa kishamba wa tz

    ReplyDelete
  6. Kilicho mfurusha Eymael ni lugha ya kibaguzi aliyoitoa kwetu sisi watanzania kwamba ni manyani na mambwa. La ubovu wa viwanja mbona lipo wazi tu

    ReplyDelete
  7. Hili wazo la kwamba mechi ya fainali ya FA ichezwe uwanja mkuu wa taifa ni wazo excellent.

    ReplyDelete
  8. Ki ukweli fainal inafaa kuchezewa viwanja 3 tuu taifa uhuru na azam tuu ni mbora wakati mashindano yanaanza yachezewe huko kwenye viwanja vibovu linapokuja swala la fainal ni utumike uwanja wenye hadhi ya fainali mpira wa tanzania unaongozwa na watu ambao sio wanamichezo ni wanasiasa unawezaje kupeleka fainal kule? hata mapato tuu unapataje? hv mpira si biashara? unajua kabisa hapa biashara inalipa halafu we unaenda sehemu hailipi? kunabwageni toka nje wanataka kuja kuangalia fainal sasa kule anafikia hotel gan na zipo ngapi nashauri mpira wa tz uongozwe na watu wa mpira

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic