July 28, 2020


MWINYI Zahera aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga amesema kuwa amesikitishwa na vitendo vya Luc Eymael ambaye amefukuzwa kazi hivi jana,Julai 27.

Yanga ilitoa taarifa kwamba imeamua kuachana na Eymael kwa kosa la kutoa kauli za kiubaguzi jambo ambalo si la kiungwana na kuomba radhi kwa mashabiki, Serikali ya Tanzania na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Zahera amesema kuwa amekia sauti ya Eymael jambo lililomsikitisha kwa kocha huyo kushindwa kuwa na nidhamu ya kazi.

"Kosa kubwa la kwanza nadhani alifanya pale ambapo walicheza nyumbani kabla ya kwenda Morogoro alikwenda kusema kwamba hataki kuwa na wasaidizi kama atakuwa anakwenda kwenye timu wawe wanabaki yeye awe anaondoka.

"Huwezi kufanya hivyo kwa sababu hilo ni suala la kuongea na uongozi kisha mambo yakaisha na sio kuzungumza tena mbele ya waandishi wa habari.

"Huwezi kupata fedha hata dola moja, Ulaya huyu kocha hawezi kupata kazi ni mtu ambaye anafanya mambo mengi ya ajabu na inaniuma kwa sababu wazungu wengi Ulaya hawana kazi anapata bahati ya kupata dola elfu sita au elfu saba Ulaya hawezi kupata hata dola efu mbili.



"Haiwezekani kocha wa mpira aseme mambo mengi ambayo ameyasema kupitia kwenye vyombo vya habari, analalamika vitu vingi mara nyumba mara Wi-fi inaonakena kwamba ni maskini hawezi kulalamika vitu kama hivyo," amesema.

Eymael ameomba radhi kwa kosa hilo kwa kueleza kuwa alifanya hivyo kutokana na presha ya kushindwa kutwaa taji la ligi pamoja na Kombe la Shirikisho. 

3 COMMENTS:

  1. Je nani bora. Zahera au huyu Mzungu. MIMI nahisi ilikuwa kosa kumuondoa Zahera ambaye alikuwa na mpaka sasa Ana mapenzi ya dhati na timu yeta na tumeyaona yote aliyofanya. Ukimwacha mke kwa ghadhabu tu mke mwenye kheri nawe basi umrejee kwa haraka asije kumuokota mwenzio ulie uje kujuta. Ikiwa Kamfanya makosa ni bora kupewa muongozi tu kwani hakuna asiyekosea. Penseli mbele Kuna risasi ya kuandika na nyuma Kuna Raba ya kufutia makosa

    ReplyDelete
  2. Huyu Zahera akae kimya yeye mbona alifanya udalali wa Makambo

    ReplyDelete
  3. Kukurupapaka za utopolo, kula siku movie mpya tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic