July 31, 2020

YANGA imedhamiria kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao ambapo mabosi wa Kamati ya Usajili chini ya udhamini wa GSM wameandaa sapraizi kubwa kwa mashabiki wao itakayofanyika katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi.

Timu hiyo imepanga kukiboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji tisa watakaoingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo msimu ujao.

Tayari wapo baadhi ya wachezaji wanaotajwa kwenye usajili wa timu hiyo, kati ya hao ni kiungo Mkongomani,Mukoko Tonombe anayekipiga AS Vita ya DR Congo, Eric Rutanga (Rayon Sports), Tuisila Kisanda (AS Vita), Heritier Makambo (Horoya AC) na Yacouba Songne ambaye ni mchezaji huru.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, rasmi kilele cha tamasha kubwa la Wiki ya Mwananchi litafanyika Agosti 9, mwaka huu ambapo siku hiyo, Yanga wataitumia kutambulisha wachezaji wao wa msimu ujao wa 2020/21.

Kati ya watakaotambulishwa ni kiungo mkabaji wa zamani Simba, Mghana, James Kotei.Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, GSM wamefanikisha usajili huo kwa asilimia mia na kilichobaki ni kiungo huyo kutua nchini kwa ajili ya utambulisho rasmi kwa mashabiki wa timu hiyo, kisha kuanza kazi.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, ujio wa kiungo huyo umepangwa kufanywa siri kubwa na mara atakapotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, kila mmoja ataamini kweli wameamua kukijenga kikosi chao.

Aliongeza kuwa, utambulisho wa kiungo huyo unatarajiwa kuwa wa tofauti na wachezaji wengine wapya watakaojiunga na timu hiyo katika kuelekea msimu ujao.

“GSM kwa kushirikiana na viongozi wa Yanga tayari wamekamilisha usajili wa wachezaji wao wapya kwa asilimia 90, kilichobaki ni nyota hao kuanza kuwasili nchini tayari kwa ajili ya utambulisho.

“Wachezaji hao watatambulishwa Agosti 9, mwaka huu, siku maalum iliyopewa jina la Wiki ya Mwananchi ambayo huitumia Yanga kutambulisha wachezaji wao watakaowatumia msimu ujao.

“Katika siku hiyo ndiyo Kotei atatambulishwa mbele ya mashabiki wa timu hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, pia siku hiyo wachezaji wengine wapya watatambulishwa sambamba na kuingia kambini tayari kuanza msimu mpya,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli, alidokeza kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya baada ya wiki mbili kuanzia sasa sambamba na kuanza kushuka kwa wachezaji wapya.

“Kuanzia Agosti Mosi, mwaka huu, mashabiki wa Yanga tarajieni kuanza kuwashuhudia nyota wa kigeni wakianza kutua nchini kukamilisha masuala ya usajili kabla ya kuanza majukumu yao,” alisema Bumbuli.

6 COMMENTS:

  1. TATIZO LENU YANGA: MNATANGAZA TANGAZA KILA MCHEZAJI MNAEFUATILIA HUU NI UDHAIFU MKUBWA SANA NA UNAWAGHARIMU SANA, FANYENI MAMBO YENU KWA SIRI SANA, MKIJUA HAMNA FEDHA MMEBAKI JINA MAARUFU TU, HAMTISHI KWANI HATA KMC ANAWEZA KUWANYANG'ANYA MCHEZAJU MNAE MTAKA SEMBUSE SIMBA NA AZAM?!!! ACHENI USWAHILI WA KUSEMA SEMA HOVYO KUWENI WASIRI.

    ReplyDelete
  2. Yanga team yangu ila the way wanavyo fanya usajiki wao kwa miaka ya hivi karibuni inasikitisha sana. DR Msolla M/Kiti ni msomi wa hali ya juu na aliwai kuwa mwalimu wa timu ya taifa, Mwakalebela amewai kuwa mtendaji mkuu TFF ila kwa jinsi wanavyo endesha mambo ni kama tuna kina Mzee Akilimali na wenziwe. Nilifurahi sana tulipopata uongozi huu mpya na naamini wanayanga woote popote tulidhani tutaona tofauti kubwa kwa aina ya majina ya viongozi tulio wachagua lkn taratibu tunaanza kukata tamaa, kiu na ndoto yetu kuona Yanga Afrika Afrika mpya inaanza kuyeyuka. Hivi niulize kama ni kweli tunayao yasoma magazetini ni kweli ni kwamba hatuna scout or weledi kutafuta wachezaji wazuri kushinda hawa ambao wa
    Wametoka or wamewai kuchezea Simba? Ombi langu kwenu viongozi wetu jitafakalini sana na mjipange vizuri mnapolekea kusajili wachezaji huku pia safari ya mabadiliko ikiendelea kwa mwendo wa jongoo. Yanga daima mbele

    ReplyDelete
  3. Muda mwingine tunaeza laumu uongozi wa Yanga lakini kumbe ni hawa watu wa Media ambao hutaka kuuza magazeti yao...Wamezoea kuropoka ropoka hata issues wasizokuwa na uhakika Nazi, mwisho wa siku tunalaum viongozi.

    ReplyDelete
  4. Yanga mnaongea sana. Mlisema mnamsajili Awesu Awesu, kisha Azam wakamchukua. Fanyeni vitendo badala ya kuchonga. Hakika Utopolo ni Utopolo tu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Enter your reply...taja kiongozi aliyesema wanamsajiri Awesu Awesu wewe siyo unaropoka tu,hizo ni media ndugu acha kujimwambafy kwa vitu usivyo na uhakika navyo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic