July 15, 2020

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa suala la Bernard Morrison kiungo mshambuliaji kurejea ndani ya timu hiyo na kuwa Kwenye kikosi kitakachowavaa Singida United leo lipo mikononi mwa benchi la ufundi.

Benchi la ufundi la Yanga linaongozwa na Kocha Mkuu, Luc Eymael raia wa Ubelgiji ambaye kwenye mchezo uliopita, Julai 12 wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba alimchezesha kiungo huyo dakika 64 na nafasi yake ikichukuliwa  na Patrick Sibomana. 

Baada ya kutolewa nje, Morrison aligoma kukaa benchi na kutoka jumla nje ambapo inaelezwa kuwa alipanda bodaboda na kusepa Uwanja wa Taifa jambo lililowakasirisha mashabiki wa Yanga pamoja na viongozi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa suala la Morrison kurejea kikosini na kambini lipo mikononi mwa benchi la ufundi.

"Kuhusu Morrison suala lake la kuwa ndani ya kikosi ama kurejea kambini  lipo mikononi mwa benchi la ufundi wao ndio watatuambia kama wanamhitaji au la kwani ndio kazi yao," amesema.

Mchezo huo Yanga ilikubali kuyeyusha tiketi ya kusonga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa mabao 4-1.

Leo Yanga inacheza na Singida United Uwanja wa Uhuru mchezo wa Ligi Kuu Bara.

10 COMMENTS:

  1. Yaani hii timu yenu ndio naana hatupati maendeleo. Mchezaji ameonyesha utovu mkubwa wa nidhamu, VIONGOZI uchwara na benchi la ufundi wanatupiana mpira kuhusu nani achukue hatua.Tukifanya mchezo masuala haya yatatugharimu sana kwenye mustakabali wa timu.

    ReplyDelete
  2. Hii ndiyo sababu mchezaji anaudharau uongozi wa Yanga. Anajua hawawezi kufanya cho chote kwake bali watamtegemea aliyemleta klabuni hapo ambaye ni kocha Luc

    ReplyDelete
  3. Watamrejesha na akiwafungia tena goli wataanza kumshangilia. Kwa upuuzi huu acha tu muendelee kupigwa 4G.

    ReplyDelete
  4. Kwani wachezaji wengine hawapo wa kufunga magoli? Mbona Fei Toto juzi kawafuta machozi. Basi tu ni utumwa wa kimawazo kumwabudu mchezaji ambaye yeye peke yake hawezi kuitwa timu ya Yanga. Wafuatilie historia yake ya kutokutumikia klabu kwa zaidi ya mkataba wa msimu mmoja kote huko alikotoka. Ndiyo sababu Luc alimpata akiwa hana timu na akiwa mchezaji huru. Kwa nini timu aliyokuwa anaichezea haikutaka kumwongezea mkataba kama kweli ni mchezaji mzuri?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nina shaka sana na afya ya akili ya Morrison au wanaomshauri

      Delete
  5. Mwaacheni awacheeze akili, lakini hajui waswahili wa pwani, hatacheza mpira mpaka kufa

    ReplyDelete
  6. Juzi alikuwa kipenzi na kuitwa muuwaji wa Simba. Hivi karibuni walianza kumzomea na leo wanasema Ana ugonjwa wa akili. Wanawavuruga nyota wao halafu wanajivuruga wenyewe

    ReplyDelete
  7. Juzi tu mlimsifia sifa zote leo mmepogwa 4G mnamuona hafai tena hao ndio GONGOWAZI bwana

    ReplyDelete
  8. Gongowazi hawana muamana.Hawana shukurani.Wamepigwa arbaa basi Morisson kawa mgonjwa wa akili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic