July 15, 2020



MTUPIAJI namba mbili ndani ya Klabu ya Lipuli, Daruesh Saliboko leo anasherehekea Siku ya kuletwa duniani huku akiahidi kuendelea kupambana kufikia malengo ya timu pamoja na yake aliyojiwekea. 

Saliboko ndani ya Klabu ya Lipuli ametupia mabao 10 huku kinara akiwa na Paul Nonga ambaye ni nahodha wake akiwa na mabao 11.

Nyota huyo amesema kuwa anaamini kwamba timu hiyo msimu ujao itashiriki ligi licha ya kupita katika kipindi kigumu cha mpito kwa kupata matokeo ambayo sio chanya.

"Bado nafasi ya kubaki kwa Lipuli kwenye ligi ipo katika mwendo wa kusuasua bado tuna amini tutabaki Kwenye Ligi.

"Malengo yangu pia yatatimia kwani baada ya miaka mitano huko mbele nina mpango wa kucheza soka la kulipwa nje ya Bongo," amesema.

Lipuli ipo nafasi ya 13 na  pointi 40 baada ya kucheza mechi 35.

1 COMMENTS:

  1. Mbona Pana kasoro hapo umesema anasherehekeai siku yake ya Kuja duniani bila ya kutaja umri huo anaousherehekea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic