July 28, 2020


MTENDAJI Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, raia wa Afrika Kusini, amefunguka kuwa watazungumzia juu ya hatima ya kiungo wao Msudan, Sharaf Shiboub, pale watakapokuwa wamemalizana kila kitu.

Shiboub tayari ameshamaliza mkataba wake wa mwaka mmoja Simba aliosaini akitokea Al Hilal ya Sudan.

Senzo ameongeza kuwa kwa sasa hawatakuwa na lolote juu ya mkataba wa kiungo huyo licha ya kwamba muda wake ndani ya timu hiyo umemalizika baada ya ligi kuisha Julai 26.

Kigogo huyo ameongeza kwamba siyo kwa Shiboub tu, bali pia hali hiyo itajitokeza kwa wachezaji wao Pascal Wawa, Yusuf Mlipili na Deo Kanda ambao wanamaliza mikataba.

Senzo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wataweka kila kitu wazi juu ya mustakabali wa wachezaji wao pale ambapo watakuwa wamemaliza kila kitu.

“Kuhusiana na masuala ya mikataba ya wachezaji tutaweka habari kwenye mtandao wetu mambo yakiwa tayari, kwa sasa kuna vingi ambavyo tunaviangalia nje ya mikataba yao.

“Huwa sipendezwi na tetesi za wachezaji wetu kutakiwa huku na kule, nilisema hilo tangu mwanzo hivyo wasubiri kuona kina nani watabakia na wataondoka kwenye kikosi chetu,” alisema Senzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic