July 17, 2020


STAA wa Barcelona, Luis Suarez amefunguka kuwa anamkaribisha kwa mikono miwili kinda wa Inter Milan, Lautaro Martinez kwani ni mchezaji bora na mwenye uwezo.

Kinda huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Barcelona kwa muda mrefu na bado haijafahamika hatma yake japo amekuwa tishio kwa msimu huu kutokana na kiwango chake.

Ujio wa Martinez ndani ya Barcelona unatajwa kuwa ndiyo mbadala sahihi wa Suarez ambaye anacheza naye nafasi moja ya ushambuliaji namba tisa.

“Kwangu ni mchezaji bora kutokana na uwezo wake
Pia kucheza Inter sio kazi ndogo kwa maana hiyo yupo levo ya juu na anaweza kupambana, namkaribisha Barca kwa mikono miwili.

“Unajua sio kazi rahisi mchezaji kutoka Argentina kwenda kucheza Italia, lakini yeye ameweza kufanya hilo kwa sababu hakuna ligi ngumu kama ligi ya Italia na yeye ameonyesha anaweza.

“Bado kwa umri ni mdogo na kama akija hapa Barcelona nitamsaidia kwa kiasi kikubwa kuenda na kasi ya hapa na kama atafanikiwa kwenye hilo basi atakuwa mchezaji bora kuliko kawaida,” alisema Suarez.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic