YANGA iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael, kesho ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa na utakuwa na ushindani mkubwa kulingana na hesabu za kila timu kuwa tofauti.
Mwadui FC inapambania nafasi ya kubaki ndani ya ligi ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake 40 huku Yanga ikihitaji kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili.
Kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 na mshindani wake ni Azam FC ambaye yupo nafasi ya tatu na pointi 65.
Eymael amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata pointi tatu muhimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment