KIUNGO mtata wa Yanga, raia wa Ghana, Bernard Morrison amesema kuwa kwa sasa ni mchezaji huru hivyo anasubiria ruhusa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ili aende kula bata la miezi miwili kwao.
Morrison alijiunga na Yanga kwenye dirisha dogo la Januari, mwaka huu, ambapo alionyesha kiwango cha hali ya juu ndani ya kikosi hicho jambo lililowafanya mashabiki wa Yanga kumpenda kabla ya kuingia kwenye mtafaruku wa mkataba wake.
Morrison ameweka wazi kwamba kinachomfanya aendelee kuwepo nchini hadi sasa ni TFF, ambao wamemtaka asubirie majibu ya madai yake ya utata wa mkataba na Yanga wanaodaiwa kumuongeza miaka miwili kabla ya ule wa miezi sita kuisha.
“Najua mashabiki wa Yanga, nimewakwaza sana, ila hilo halinisumbui sana maana ninachofanya ni kuhitaji haki yangu na kupunguza mambo ambayo yanataka kuniharibia maisha yangu.
“Kutokana na hilo sasa naisubiria TFF pekee inipe majibu yangu kisha nikapumzike kwetu Ghana.
“Sina mpango tena wa kurejea Yanga, maana uongozi siuelewi kabisa hadi leo hii nawadai mishahara yangu ya miezi miwili hawajanilipa.
"Sijui tatizo nini au ndiyo kisa cha kunilazimisha nimesaini mkataba wakati mimi natambua ule wa miezi sita tu, ngoja niende zangu Ghana nikapumzike,” alisema Morrison.
Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuhusu suala hilo alisema: “Nafikiri jambo zuri unalotakiwa kumwambia ni akupe slip zake za benki uone kama kweli anamaanisha, mwambie aache maneno yake ya ajabu.”
Chanzo:Championi
Hapi hakuna mchezaji. TFF wawe makini wasijichafue bure
ReplyDeleteHuyu mtu angeshtakiwa kwa utapeli ili liwe fundisho kwa wengine. Haimtoshi kuichafua Yanga na TFF ataichafua nchi pia
ReplyDeleteYanga ni nchi?
DeleteHayo ndio matokeo ya kudhulumu wachezaji Tambwe, Dante, Chirwa, pondamali, Zahera wote wanadai pesa
ReplyDeleteDah ngoja tuangalie mwisho wa hili tatizo la mkataba! maana naisi km kuna janja janja vile! Hivi inawezekana kweli mchezaji apewe mkataba na pesa za kusaini apewe alafu aseme hana mkataba kweli? NGOJA TUONE
ReplyDeleteAnalichafua Taifa lipi?Wajibikeni na matatizo yenu msilihusishe Taifa. Morisson hata mara moja hajasema na mgogoro na TFF wala Nchi. Amesema aba matatizo na Yanga.Tulitafutie ufumbuzi tatizo hili kama Yanga.Tuache blame game.
ReplyDeleteujue viongozi wetu wanapenda kucheza na mashabiki ili tu waaminike kuwa wao ni wachapakazi, najua kabisa wao viongozi pia walitutangazia kuwa tayari wamemalizana na Tshishimbi lakini leo hii Tshishimbi hana mkataba hivi kweli hapa tutalaumu wachezaji? mimi naona VIONGOZI wanataka kutumia fulsa kwa wachezaji kwa kutuaminisha kuwa wao ni wazalendo wa yanga kumbe hapa huwa wanatafuta kick, la msing viongozi wetu wafanye kazi bila mihemko ya mashabiki kama huwezi kununua kununua nyama nunua dagaa, usione jirani yako anakunywa kila siku chai ukataka nawe unywe utaingia kwenye mgogoro wa madeni maana unataka uishi kama jirani kumbe tayari uwezo kakuzidi ebu Yanga tujipange upya Simba wametutangulia na tukubali ndo tutafanikiwa. VIONGOZI tuache kufanya mihemko kwa ajili ya kuridhisha mashabiki tutaendelea kuumbuka.
ReplyDelete