July 18, 2020


OWEN Chaima kipa namba moja ndani ya Klabu ya Singida United amesema kuwa anamuombea dua nyota wa Yanga, Ditram Nchimbi afike mbali Kwenye maisha yake ya soka.

Chaima amesema kuwa anaamini uwezo wa Nchimbi ni mkubwa hivyo akipambana zaidi anaweza kufikia malengo yake aliyojiwekea.

Walipokutana Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Singida United ilikubali kichapo cha mabao 3-1.

"Ninamuombea kheri Nchimbi ni mchezaji mzuri nina amini atafika mbali akiongeza juhudi," amesema.

Singida United tayari imeshashuka daraja baada ya kujikusanyia pointi 15 kibindoni leo ina kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic