July 26, 2020


UWANJA wa Samora mchezo Ligi Kuu Bara kati ya Lipuli na Yanga ni umekamilika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mashabiki wamejitokeza kuona burudani ya mwisho ndani ya Uwanja Samora. 

Matokeo hayo yanawafanya wachezaji wa Lipuli watoke uwanjani wakiwa na huzuni timu ikishuka rasmi daraja.

Bao pekee la ushindi lilipatikana dakika ya 38 likipachikwa kimiani na David Molinga.

Ushindi huo unaifanya Yanga imalize ligi ikiwa nafasi ya pili na pointi 72 huku Lipuli ikikata tiketi ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza  wakiwa na pointi 44.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic