July 26, 2020


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Simba umekamilika kwa Simba kushinda mabao 2-1 Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Kabla ya mchezo wachezaji walitoa heshima kwa kusimama kwa muda wa dakika moja kwa ajili ya kumpa heshima Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.


John Bocco dakika ya pili alifunga kwa Simba na Polisi Tanzania iliweka usawa dakika ya 32 kupitia kwa Marcel Kaheza kwa penalti.

Bocco alifunga bao la pili dakika ya 45 na kuifanya Simba isepe na pointi tatu mazima Uwanja wa Ushirika.

Simba inajiongezea pointi tatu na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 88 huku Polisi Tanzania ikibaki nafasi ya tano na pointi zake 55.

2 COMMENTS:

  1. Simba wameshachukua ubingwa. Polisi hawashuki daraja. Ingekuwa vyema leo ungeweka mechi za wanaopigania kubaki ligi kuu na wale wanaotafuta nafasi ya pili. Au we unaonaje Saleh?

    ReplyDelete
  2. Tuwekeeni timu za chini ndiyo kuna msisimko.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic