August 13, 2020

Mghana Bernard Morrison ambaye amesaini dili la miaka miwili Simba, amesema mashabiki wa timu yake hiyo mpya wasiwe na wasiwasi kwani hatakuwa na usumbufu kama waliouona akiwa Jangwani.

 

Mghana huyo amesema kuwa kilichomvutia kutua Simba ni ubora wa kikosi walichonacho, wakiwa na viungo Clatous Chama na Luis Miquissone, pia anataka kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao.

 

“Kabla ya kusaini Simba niliangalia baadhi ya vitu vikiwemo suala la ubora wa kikosi cha sasa cha hapa, kitu ambacho kimenishawishi kujiunga nao kwa ajili ya kufanya nao kazi kwa msimu ujao.

 

“Lakini pia mimi kama mchezaji nina malengo yangu ya kutaka kucheza kimataifa na Simba wanayo nafasi hiyo, ndiyo maana nikaona kuna umuhimu wa kujiunga nao kwa ajili ya kuonekana zaidi msimu ujao,” aliweka nukta Mghana huyo.

 

Nyota huyo Mghana wakati akiwa Yanga anakumbukwa kutokana na matukio yake kadhaa ya utata ambapo baada ya kutua Simba amefunguka kuwa atatulia na kuwaahidi mashabiki wa klabu hiyo kutazama kile ambacho atakifanya uwanjani na kuachana na masuala yaliyopita.

 

“Mashabiki wa Simba kwa sasa wanachotakiwa kufanya ni kuangalia kile ambacho nitaenda kufanya nikiwa kwao na siyo masuala yaliyopita. Watazame kile ambacho nitaenda kukifanya nikiwa uwanjani kwa ajili ya timu yangu,” alimaliza Morrison.

21 COMMENTS:

  1. Ni ahadi nzuri na za kutia moyo hasa pale hakukanya binafsi kuwa vile aliwatesa matajiri wake wa zamani na muungwanana anapokiri makosa yake huwa hayarejei tena na pia namsifu kwa uungwana wake kuwa hakuwataja Hao aliowakataa kwa ubaya wowote jambo ambalo wengi hufanya. Kaondoka kwa amani na kuahidi hayo aliyoyatenda huko hatoyatenda kwa timu yake mpya na kuyataja yale yaliyompeleka huko kupya Bila ya kutoka roho kwa kipato zaidi au kuisema timu yake ya zamani kwa ubaya wowote. Ama kwa hapo namsifu na kumtakia kila la heri na ni juu ya timu yake ya zamani kutomsakama kwa kwa maneno makali na kuyasahau na kusameheana yaliyopita na kutazama yanayokuja na hizo ndizo sifa za kuungwana

    ReplyDelete
  2. Anajua huko Kuna mpunga Na atashiriki mashindano makubwa

    ReplyDelete
  3. Mimi upande wangu napenda mtu kuwa Mungwana,lkn hapa tatiZo ni media Mr salehe wewe Ni shabiki wa Simba na kwa kuthibitisha Hilo unapenda kuandika vipande vingi vya habari kuhusu Simba mtu anaongea dk kumi wewe sasa unakuwa wakala wa kuongeza utamu hata sisi wasomaji tunajua mtiririko was taarifa hacha kuwa mfafanuzi was taarifa za Simba ,ya Morrison yaliisha Jana.Mbona Mwamnyeto mlipoambiwa la sign Yanga mkamchunia?

    ReplyDelete
  4. Akija mchezaji mzuri Yanga mnaanza kujenga naye urafiki mpaka kumpeleleza then. Mna muunganisha na Simba yote tunayajua

    ReplyDelete
  5. Kawaida ya Utopolo. Singizia wengine. Tatizo sio la Utopolo ni la wengine. Viongozi wabovu hawaoni. Andika mkataba mbovu, futa sehemu kwa jslamu,chana sehemu ya mkataba sio kosa la Utopolo bali la Saleh Ally na Simba.
    Take responsbility.Watu sio wajinga. Unaweza kuwaongopea watu mara moja lakini huwezi kuwaongopea watu kila mara. Tshimbishimbi amesaini deal done.Baada ya mwezi tunampa wiki 2 asaini. Baada ya wiki wamemuacha.Taasisi inaendeshwa kihovyo. Wanatafuta scapegoat kwenye kila jambo. Inferiority complex na offer mentality.

    ReplyDelete
  6. Morrison sio mkweli, yupo kimaslahi zaidi,
    Ukiangalia series yakeutagundua hilo:-
    1- akivyokuwa Yanga alisema Simba wanamsumbua, Ili kujenga hisia yakumuonfeza mpunga,
    2- alisema hajasaini mkataba wakati alisaini sema mkataba ndio unaKasoro ndogo ndogo kwa mujibu wa Kamati,
    3- kama kwweli yeye sio mtovu wa Nidhamu Kwann hakupata team Ghana mpaka Yanga ndio Waka masajili kwa miezi sita,
    Ninavyoona. Mimi huyu hata Simba atasumbua ni suala la muda tu,
    Kwa sababu kauli zake zinabadilika kila siku.

    ReplyDelete
  7. Tahasisi nzuri we zuzu darasa la Saba Senzo kaondoka tahasisi ipi?kwa Uelewa wako unadhani Uongozi unapimwa kwa kwa huyo mchezaji mmoja,?Kuna siku niliwahi kuongea kuwa watu maskini wa akili na wachawi huwa fikra zao nyepesi,kwahiyo kwako wewe unataka kutwambia kuwa Viongozi wa Yanga kazi yao Ni Morrison na Tshishimbi then.Mnajivika uandishi lkn ndani na rohoni mwenu wanafiki

    ReplyDelete
  8. Responsibility inapimwa kwa Hilo tu?ungekuwa mkrsto ningekwambia Soma habari za Sodoma na Gomora na habari ya Ruth and co .CEO kakimbia TFF Mali yao , Kamati yao Redio zao ,maga Maga zeti yao ,unahitaji uwajibikaji kwenye ushetani??

    ReplyDelete
  9. Leo Redio zote ni Simba day,je kwa Wingereza mfano kila kitu ni Liverpool

    ReplyDelete
  10. Hoja hujibiwa kwa hoja.Jibu hoja wacha kusingizia ushetani kama kawaida yenu.Senzo hakukimbia Alitaka mshahara mkubwa zaidi akajibiwa kwamba kwenye majukumu aliyopewa kwenye mkataba wake hau justify kuongezewa mkataba.Akasepa. Alifanya hivyo skiwa Orlando Pirates sio jambo la ajabu. Kosa la kiuweledi alilofanya ni kutokabidhi ofisi kwa muda baada ya kuondoka. Mwisho umeropoka tu kama mtu aliyechanganyikiwa.

    ReplyDelete
  11. Fungua Wasafi usikie uzao wa Watoto waliofichwa vyumbani ,ni Simba na Yanga tu ndo Elimu yetu

    ReplyDelete
  12. Tahasisi ndio nini?Ni kilugha au?

    ReplyDelete
  13. Kwani mpaka Senzo analetwa hiyo board si iliridhika na CV zake ,?kwa hiyo hapa issue ni nini ?hayo unayosema wa2 wa Simba wanayajua mtu Aki apart nao?na je kwa nini Magazeti ya Champion na extra yamekuwa yakimsifia Sana akipewa kurasa mbili(ninayo) na Mwanaspoti na Ushishimbi ndo watu was maana kwenu?unataka hoja zipi? Au Elimu ndogo ???

    ReplyDelete
  14. Tahasisi/nilimaaniasha institute zaidi institution

    ReplyDelete
  15. Sasa tunajipanga kwa ubingwa. Kitu muhimu ni nyota bora tuliokuwa nao. Nyie mikia hamtuwezi si mlikuwa mnajivunia Sinzo aliekuleteeni mafanikio Jee yuwapi sasa. Tunakungojeeni kwa hamu

    ReplyDelete
  16. Senzo mtamfukuza baada ya kipigo. Nyie ngebe tu.Mkianza kuchapwa mtawatimua hao mnaowasifia.Mlisajili 22 na bado hamkuchukua hata kikombe cha babu.Timu inascha manahodha wote wawili eti iwe na chemistry baada ya mwezi 1.Wishfull thinking. Mtafeli tena halafu mtakuja na visingizio as usual.

    ReplyDelete
  17. Mnajioanfa kila msimu na gepu linazidi kuongezeka. Timu inachukua ubingwa bado mechi 6 halafu bila aibu unajifanya mshindani Puuuu.

    ReplyDelete
  18. Huyo watamtimua pale watapoanza vichapo vya mfululizo ka ilivokuwa msimu huu uliopita

    ReplyDelete
  19. Hatufungwi tumeondoa virus inaitwa Usimba ,na ndo wachezaji mmekuwa mnawatumia ku tu weaken ndo maana mna lalamika wao kuachwa

    ReplyDelete
  20. Mtu anaacha mke wewe unalaumu na kumsifia tena stena sifa za kimaumbile eg ana kovu kitovuni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic