August 4, 2020


INAELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu anaweza kutolewa kwa mkopo kukipiga ndani ya Klabu ya KMC.

Ajibu alijiunga na Simba kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Yanga hajawa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza kilicho chini ya Sven Vandenbroeck.

 Akiwa Yanga kwa msimu wa 2018/19 ametoa jumla ya pasi 17 na alikuwa kinara ila msimu huu ndani ya Simba ametoa pasi tano.

Kinara wa kutoa pasi ndani ya Simba msimu huu ni Clatous Chama ambaye ametoa pasi 10 za mabao. 

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa suala la wachezaji watakaochwa itawekwa wazi. 

4 COMMENTS:

  1. Duh! Huyu jamaa mbona mpira umekwisha mapema sana! Alikataa ofa ya TP Mazembe. Halafu mbaya zaidi anaonekana mzee kuliko umri wake. Kweli soka ni mchezo Katili.

    ReplyDelete
  2. Yanga wanawapiga misumari hao. Wachezaji wote waliotoka Yanga msimu uliopita Simba inawaacha. Kakolanya anatolewa kwa mkopo Azam, Gadieli anaachwa, na Ajib ndio hivyo tena.

    ReplyDelete
  3. Naona unajifanya bodi ya Simba Umeshajua uamuzi utakaotolewa Hongera.

    ReplyDelete
  4. Duuu, ! Sema wakala wake sound!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic