August 4, 2020


SALIM Abubakar maarufu kama Sure Boy anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ambao wanahitaji kuboresha kikosi chao msimu ujao.

Dirisha la usajili limefunguliwa na tayari kazi imeshaanza kwa Yanga wakiwa wamamalizana na wachezaji wanne ambao ni Wazir Junior wa Mbao ambaye ni mshambuliaji.

 Bakari Mwamnyeto aliyekuwa akikipiga Coastal Union yeye ni beki, Zawadi Mauya aliyekuwa anakipiga Kagera Sugar na Yasin Mustapha aliyekuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania.

 Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa miongoni mwa nyota watakaotambulishwa hivi karibuni ni pamoja na Sure Boy.

"Sure Boy yupo kwenye hesabu za Yanga na muda wowote anaweza kutambulishwa hivyo ni suala la kusubiri wakati," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi hicho hivyo watafanya usajili makini.

"Tupo makini katika masuala ya usajili hatukurupuki ila wakati ukifika lazima tutaachia mchezaji mwingine," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic