CRIS Mugalu mshambuliaji aliyekuwa anakipiga ndani ya Power Dynamo ya Zambia, leo Agosti 16 ametambulishwa ndani ya Simba.
Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili na anaungana na washambuliaji wawili tegemeo ndani ya Simba ambao ni John Bocco na Meddie Kagere.
Bocco na Kagere wamekuwa na pacha nzuri msimu wa 219/20 ambapo wote wapo Kwenye kikosi bora cha msimu.
Kwa pamoja wamehusika Kwenye mabao 31 kati ya 78 yaliyofungwa na Simba ambayo imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kagere alifunga mabao 22 na Bocco alifunga mabao 9 hivyo nguvu ya ushambuliaji inaongezeka kwa Mabingwa hao wa Ligi mara tatu mfululizo.
This is simba BROTHER
ReplyDeleteHuyo ni sawa na YIKPE Aliechamka kidogo, kiufupi mmekula za uso hapo hamna mshambuliaji
ReplyDeleteMfungaji bora Zambia wakati huyo Yipke wako bomu hakuwai kuwa mfungaji bora sehemu yoyote ile duniani tangu azaliwe na hatokuwa mpk atakufa
ReplyDeleteHuu usajili simba mtaua jamani kha, au mnataka kwenda kushiriki ligi ya Spain? Tangu lini sisimizi akauliwa kwa shoka?
ReplyDeleteKaribu kwa mabingwa Mugalo
ReplyDeleteMchezaji anaitwa Chrispin MUGALU sio MUGALO. Timu aliyotoka ni LUSAKA DYNAMOS na sio POWER DYNAMO. Msichanganye mambo nyie waandishi.
ReplyDeleteTshishimbi vipi jamani? Maana wachezaji wa kimataifa ndio washaisha hivyo!
ReplyDelete