Sven Vandenbroeck Kocha Mkuu wa Simba ndani ya ardhi ya Bongo Agosti 16 kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji msimu wa 2019/20 ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa msimu akiwapoteza Hitimana Thiery wa Namungo FC na Arstica Cioaba wa Azam FC.
Mkononi alitwaa mataji mawili, Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara ambapo alilikuta taji la ngao ya jamii walilitwaa Simba kutoka kwa mtangulizi wake Patrick Aussems maarufu kama Uchebe.
Sven amesema anafurahi kurejea Tanzania huku kuhusu mipango ya timu akisema kuwa atazungumza Jumanne.
0 COMMENTS:
Post a Comment