KLABU ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima, kwa mkataba wa miaka miwili.
Kiungo huyo alikuwa kwenye rada za Yanga ambao inaelezwa kuwa walikuwa wamefika naye hatua nzuri ila mambo yakawa magumu kwenye upande wa dau la nyota.
Inaelezwa kuwa Niyonzima alikuwa anahitaji milioni 11 na Yanga mkononi walikuwa na milioni nane jambo lililofanya nyota huyo aibukie kushoto na kudakwa na Azam FC.
Niyonzima alikuwa akicheza Rayon Sports ya Rwanda, usajili wake ni sehemu yamapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.
Kiungo huyo amesaini mkataba leo, Agosti Mosi, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
Niyonzima, yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi', anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao.
Usajili wa kwanza ulikuwa ni wa kiungo Awesu Awesu, kwa usajili huru akitokea Kagera Sugar.
Mm ni simba lakini azam ni mwenzetu nampongeza kwa kuweka mambo hadharani kama hivi mchezaji wa pili anasainishwa tunaona live nimependa sana hivi huku kwetu magazeti tu hadi tunachanganyikiwa hatuelwi tunasajiri kwa magazeti jamani hata mkinichukia nasema ukweli na mm ni mwanachama wa muda mrefu sana tuige azam wanaonyesha mfano sio vichwa vya magaeti ya uwongo tumechoshwa. Hata GONGOWAZI wamemuonyesha mwamnyeto anasaini leo na mlisema wetu mmemalizana nae haya sasa GONGOWAZI wamemsainisha tunaona sasa tubadilike tuache uwongo jamani tusonge mbele
ReplyDeleteMwana Simba mwenzangu punguza pressure!! Kwanza nikupe taarifa HAKUNA KIONGOZI YOYOTE YULE WA SIMBA SC ALIYESEMA TUMEMALIZANA NA MWAMNYETO NARUDIA HAKUNA. Pili Manara alisema msimu huu SIMBA ITASAJILI WACHEZAJI WANNE TU!!!! WAWILI WA NDANI NA WAWILI WA NJE, MMOJA TAYARI WA NDANI NI ILAMFIYA WA KMC. TULIA KIONGOZI MAMBO YETU BADO NA YANAKUJA
DeleteMchezaji gan milion 11
ReplyDelete11 ni mshahara wa mwezi siyo ada ya uhamisho.
Deleteharuna anahangaika tu, atamaliza team zote bonge na kuambulia zero mafanikio
Delete