August 14, 2020

 



TIMU ya Ruvu Shooting Star yenye maskani yake Pwani (Barcelona ya Bongo), leo, Agosti 14, 2020, imeingia mkataba na Kocha mpya, Charles Boniface Mkwasa (Master), ambaye atakuwa Kocha Mkuu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa ni maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2020/21 ili wawe imara ndani ya uwanja.

Mkwasa amechukua mikoba ya Salum Mayanga aliyekuwa akikinoa kikosi hicho msimu wa 2019/20.

"Tunaimarisha kikosi na kuboresha benchi la ufundi, amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Barcelona ya Bongo," amesema.

Kabla ya kuibukia ndani ya Ruvu, Mkwasa alikuwa akikinoa kikosi cha Yanga na aliomba ajiweke pembeni baada ya msimu wa 2019/20 kukamilika.

2 COMMENTS:

  1. Mwandishi vipi, mara Ruvu shooting mara mtibwa, kuwa makini

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa vizuri afisa habari wa Mtibwa kuzungumzia mipango ya Ruvu Shooting wakati Ruvu ina msemaji wake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic