BAKARI Mwamnyeto beki kisiki wa Coastal Union leo Agosti Mosi amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Yanga.
Nyota huyo alikuwa kwenye rada za mabosi wa Yanga kwa muda mrefu ambapo walikuwa wakivutana kwenye upande wa maslahi.
Baada ya kufikia makubaliano mazuri kwa pande zote mbili kati ya Yanga na mchezaji pamoja na uongozi hatimaye leo amesaini dili la miaka miwili.
Akiwa Coastal Union alikuwa ni nahodha ambaye ameongoza kikosi chake kumaliza ndani ya 10 bora .
Kwenye msimamo kipo nafasi ya 7 baada ya kucheza mechi 38 kimefungwa mabao 30 huku ikifunga jumla ya mabao 33 naye akitupia bao moja.
Kila la kheri, maslahi ya mchezaji ni muhimu zaidi na uhakika wa kupata namba
ReplyDeleteTunatoa taadhari mwamnyeto usije lalamika huko mbele ,unadai mishahara yako.
ReplyDeleteAcha fikra mgando, ameridhika na masharti ya mkataba....
ReplyDeleteKilichompeleka yanga ni ule udhamini wa gsm kwa coastal. Hawezi kudumu pale
ReplyDeleteKwani lazima utoe comments za ajabu?unaweza kusema mungu akujalie na maisha mema
ReplyDeleteHongereni yanga
ReplyDeleteAsante sana
Delete