August 12, 2020

 

UONGOZI wa Gwambina FC umesema kuwa nafasi ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga ndani ya timu hiyo ni kiongozi wa masuala ya ufundi (Technical Director) na hawana mpango wa kubadilisha benchi la ufundi.


Zahera aliwahi kuinoa Yanga msimu wa 2018/19 na alimaliza Ligi Kuu Bara timu ikiwa nafasi ya pili, alianza msimu wa 2019/20 na timu ila alipigwa chini kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Katibu Mkuu wa Gwambina FC,  Daniel Kirahi, amesema kuwa wamemleta Zahera kwa kuwa ana uzoefu na masuala ya mpira pamoja na ligi ya ndani.


"Makocha wetu wanabaki ndani ya Gwambina, hakuna ambaye anafukuzwa kwani Zahera amekuja kuwa Kwenye majukumu mengine yeye ni Technical Director ndani ya timu yetu.


"Kuhusu mkataba amepewa mkataba wa awali mambo yatakapokuwa sawa tutajua tutampa mkataba wa miaka mingapi ndani ya Gwambina, " amesema. 


Gwambina FC kutoka Mwanza imepanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2019/20 na 2020/21 itashiriki Ligi Kuu Bara.


Makocha walioipandisha timu ni Fulgance Novaltus na Athuman Bilal maarufu kama Bilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic