Wadau wa michezo wamekuwa wakilifuatilia jambo hili na nchi nzima kiujumla kwa ukaribu, haya huu hapa mtazamo wa Saleh Jembe kuhusu namna wadau wanavyolifuatilia kwa ukaribu pamoja na maswali anayojiuliza:- Nimeona UMMA uliokuwa ukijaa pale nje ya TFF, nikajiuliza mambo mengi na kuogopa kabisa UPENZI wa mpira kupindukia.
NAJIULIZA...
1. Wale watu wameenda kazini kweli?
2. Nini kinawachanganya kuhusu Morrison?
Kweli kila mtu angependa haki itendeke lakini naona kama TUNAMKWEZA Morrison lakini pia naona Kamati ya Hadhi za wachezaji INALIKUZA SANA hili.kusuasua kufikia uamuzi, inafanya ongezeko la watu na 'attention' ndio inaongezeka.
Jamani sisi ni Watanzania na kuna kila sababu ya kujifunza kwa hili. TUNAPOTEZA muda mwingine sana lakini LITUFUNZE kuwa makini katika mikataba, wachezaji wawe na wanasheria wao wakati wa kusaini mikataba na upande wa klabu hali kadhalika.
TUACHE kuichukulia poa mikataba na badala yake wakati wa kusaini kuwe na weledi.
Yanga na Morrison wasingelumbana leo haya yasingekuwepo na muda UNAOPOTEA sasa, tungetafakari maendeleo ya mchezo wa soka nchini.
Tujifunze kubadilika kupitia hili... Hata kama itakuwa kidogo...
Salehe bado wewe ni mdogo sana.Tunaoishi nje ya Tanzania tunajua kwanini suala Morrisson linakuzwa. Niwape pongezi tu TTF.Kwa kifupi tu wakati huu za hekaheka za kisiasa mambo kama haya ya akina Morrisoni ni sawa na kuchukua maji na kwenda kuumwagia kwenye moto unaotaka kuleta madhara.
ReplyDeleteAcha ufara we kuishi nje ndo unaungamkono upuuzi unafanywa na TFF, kwenye hili la morrison nikwamba Yanga,morrison mwenyewe na TFF, Wote wana matatizo.Niambie ni nchi gani kwel kama uko nje ya nchi umewahi kuona upuuzi kama huu unaondelea hapa Tanzania kwenye soka letu.
ReplyDelete