August 15, 2020

 

HASSAN  Mwakinyo, bondia wa ngumi za kulipwa Mtanzania anayeipeperusha vema Bendera ya Taifa kwenye ndondi, usiku wa kuamkia leo amemnyoosha kwa pointi Tshibangu Kayembe raia wa Congo.

Mwakinyo ameshinda kwa pointi pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Super Welter katika kuwania mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBF.  

Mabondia hao walionekana kukamiana na kushushiana vitasa vikalivikali katika pambano hilo lililofanyika Ukumbi wa Mlimani City Dar na kuhudhuriwa na wadau wengi.


Baada ya ushindi huo mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alimvalisha Mwakinyo mkanda huo na kumtawaza Ubingwa mpya wa mkanda huo wa WBF.

Waziri Shonza amesema anampongeza Mwakinyo kwa kuutetea mkanda huo uliopambaniwa nyumbani na kuiletea nchi sifa.

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Group, Saleh Ally, wachapishaji wa magazeti ya michezo ya Spoti Xtra na Championi ambao walikuwa ni wadhamini wa pambano hilo amesema kuwa Mwakinyo anastahili pongezi kwa kupambana na kupata ushindi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic