BAADA ya Klabu ya Yanga kupitisha panga na kuwaondoa kikosini zaidi ya wachezaji 14 waliokipiga na timu hiyo msimu huu, aliyekuwa kocha wa Yanga, Luc Eymael ameibuka na kusema maamuzi hayo yalikuwa na mapungufu.
Kocha huyo ambaye amefungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania ameeleza kuwa katika usajili huo yamepitishwa baadhi ya majina ya wachezaji ambao yeye aliona hawastahili kusalia huku pia kukiwa na wachezaji walioachwa ambao walipaswa kuondoka.
Yanga imekuwa ikikosolewa kwa maamuzi yake ya kuachana na baadhi ya wachezaji waliofanya vizuri msimu huu kama vile; David Molinga ‘Falcao’, Patrick Sibomana, Juma Abdul na Kelvin Yondani.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymael kutoka kwao Ubelgiji alisema kuna baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ambao walijitolea zaidi lakini anashangaa kwa nini wameondolewa kikosini.
“Nimepata taarifa kuwa Yanga wameachana na zaidi ya wachezaji 14, nisingependa kuliongelea sana suala hili lakini kwa mtazamo wangu nadhani maamuzi haya hayapo sahihi kwa asilimia zote.
“Kama ningesalia kuwa kocha wa kikosi basi naamini ningekuwa na mawazo tofauti kwani ningeendelea kubaki na baadhi ya wachezaji walioachwa na kuwaondoa waliopo kikosini hivi sasa.
“Tayari nimeongea na Molinga kuhusiana na suala hili lakini kama ambavyo nimesema siwezi kuingilia sana maamuzi ya watu wengine,” alisema Eymael.
Wewe ndugu huyu jamaa kakupa,nini wasaidieni Simba wampate Kama Morrison sisi hatumtaki
ReplyDeleteSimba inahusika nimi na uozo wenu.Anazungumza Luc Eymael aliyewaira nyani ba mbwa mjibuni yeye.
ReplyDeleteHalafu wanalalamika wametukanwa kumbe wameambiwa ukweli
DeleteHapa Luc Eymael kaongoea au mwandishi kaandika,kwasababu mwenye blog Ni mikia Fc awasaidie Kama alivyozoea mchukueni kwenu .Huyo jamaa kamjaza kwenye Gazeti la Champion je Kocha ndo kamtuma?kuwa na simu ukatuma maoni tu ilimradi haimaanishi una akili.hayo maoni mtumie mke/mmeo maana ndo mnadanganyana na anakuamini tu.
ReplyDeleteRudia kuandika ili tuelewe.
ReplyDeletekumbe usajili unaofanywa sii mapendekezo ya kocha!
ReplyDelete